Written by ibnially // 23/12/2012
Na Masoud Ali na Hemed Mazrouy
KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF MAALIM SEIF SHARIFU HAMADI AMETOA PONGEZI KWA RAISI WA JAMUHURI YA MUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA MRISHO KIKWETAE KWA UWAMUZI WA KUTOA FURSA KWA WA TANZANIA JUU YA KUUNDWA KWA KATIBA MPYA YA TANZANIA, JAMBO AMBALO HALIKUWAPO KATIKA TAWALA ZILIZOPITA.
MAALIM SEIF AMBAE PIA NA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBARI AMEZITOA PONGEZI HIZO LEO WAKATI AKIWAHUTUBIA WAZANZIBAR, WAFUASI NA WAPENZI WA WA CHAMA CHA WANANCHI CUF KATIKA UWANJA WA DEMOKRASIA KIBANDA MAITI IKIWA NI MKUTANO WA MWISHO KWA MWAKA 2012.
AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO AMEWAPONGEZA WAZANZIBARI WOTE KWA UMOJA NA USHIRIKIANO WAO WALIO UWONESHA WAKATI WA MCHAKATO WA KURATIBU MAONI YA JUU YA KUUNDWA KWA KATIBA MPYA YA TANZANIA.
MAPEMA MAALIM SEIF AMEBAINISHA KUWA KULIKIKUA NA MBINU NYINGI ZA KUWATOA WALE WOTE WENYE NIA NJEMA NA ZANZIBAR LAKINI KWA UIMARA WAO NA UMOJA WAO HAWAKUYUMBA LICHA YA KWAMBA WAPINZANI WALIJITAHIDI KUJENGA HOFU KWA KUWATUMIA ASKARI WA FFU NA BAADHI YA MASHEHA KUWARUBUNI WANANCHI KWA KUWAPA SHILINGI ELFU TANO.
AIDHA MAALIM SEIF AMEFAHAMISHA KUWA TANGANYIKA INA LENGO LA KUIBANA KIUCHUMI ZANZIBAR KWANI WAO WAMEICHUKULIA KAMA NI SEHEMU YA KOLONI LA TANGANYIKA NA NDIO MAANA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKAWEZA KUTAMKA WAZI KWAMBA ZANZIBAR SIO NCHI, LAKINI KWA SASA ZANZIBAR NDIO INADAI MAMLAKA YAKE KAMILI ILI KUWEZA KUJIENDESHA WENYEWE, WALA SIO JAMBO GENI KWANI HAKUNA UKOLONI WA KUDUMU.
VILE VILE MAALIM SEIF AMEWATHIBITISHIA WANANCHI KWAMBA JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZIMEAHIDI ZITASIMAMIA MAAMUZI NA MAONI YA WAZANZIBAR BILA YA UPENDELEO, HIVYO AMEWATAKA VIJANA WASIKUBALI KUREJESHWA KULIKO WALIKOTOKA KWA NI WAPINZANI WANA LENGO LA KUHARIBU HALI HII YA SIASA ILIOPO ZANZIBAR KWA SASA.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment