Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar 21/12/2012
Jamii imeshauriwa kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono kabla na baada ya kula sambamba ba kuhifdhi vinyesi sehemu stahiki ili kuweza kujikinga na maambukizi ya maradhi ya kuharisha na kutapika.
Ushauri huo umetolewa na Afisa wa Kitengo cha Kudhibiti,kuzuia na kufuatilia nyenendo za maradhi kutoka Wizara ya Afya Ali Ahmada Ali katika Semina ya kuwajengea uelewa wa maradhi ya maambukizi Wanahabari iliyofanyika Ukumbi wa Elimu mbadala Rahaleo mjini Zanzibar.
Amesema maradhi ya kuharisha bado yanaendelea katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar hivyo jamii inapaswa kuchukua tahadhari ya kujikinga na maaradhi hayo ya kuambukiza.
Ali amesema utafiti unaonesha kuwa kunawa Mikono kabla na baada ya kula kunapunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya maradhi ya kuharisha kwa Asilimia 40 na hivyo kuitaka jamii isipuuzie tabia hiyo.
Hata hivyo amesema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha maradhi hao hayasambai kwa kutoa elimu mbalimbali sambamba na kuendesha programu za dharura kwa jamii kupunguza maradhi hayo.
Hata hivyo amesema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha maradhi hao hayasambai kwa kutoa elimu mbalimbali sambamba na kuendesha programu za dharura kwa jamii kupunguza maradhi hayo.
Awali akitoa mada katika Semina hiyo Afisa wa Kitengo cha Afya na Mazingira Forogo Mtande amewataka Waandishi wa habari kusaidia kuelimisha jamii namna ya kujikinga na Maradhi hayo.
Aidha amezitaja athari zinaoweza kupatika kutokana na Ugonjwa wa kuharisha kuwa ni pamoja na kupunguza uchumi wa familia na taifa kwa ujumla kutokana na kusababisha utegemezi kwa waathirika.
Forogo ametaja athari nyingine kuwa ni pamoja na kuigharimu Serikali kutokana na kutumia fedha nyingi kwa matibabu na kudumaza sekta ya Elimu kutokana na maradhi hayo kushambulia sana Watoto waliochini ya umri wa miaka saba.
Kwa upande wao Wanahabari hao walikitaka kitengo hicho cha Afya kufanya programu za elimu kwa jamii kila mwanzo wa msimu wa Mvua ili jamii iweze kupata tahadhari mapema kabla ya maambukizi kuanza.
Pamoja na kuendelea kwa maradhi ya kuharisha na kutapika Zanzibar taarifa za Wizara ya Afya zinasema hakuna ugonjwa wa Kipindupindu Zanzíbar tokea mwaka 2009 hadi sasa.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
Chanzo: Mjengwa
No comments :
Post a Comment