Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 6, 2013

e-government in action in ZANZIBAR!


DR SHEIN: ZANZIBAR INAJIUNGA RASMI NA MFUMO MPYA WA KUENDESHA SHUGHULI ZAKE.

Written by   //  06/01/2013
Rais wa Zanzibar na Mweenyekiti wa Barza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed amesema Uzinduzi wa Mradi wa Serikali Mtandao E-Government umefungua ukurasa mpya katika uendeshaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na utekelezwaji wake utaakisi lengo kuu la Mapinduzi ya Zanzibar la kuwakomboa Wananchi kimawazo na kiuchumi.
Rais Shein ameyasema hayo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Mradi huo iliyofanyika Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Amesema lengo la Mradi wa E-Government ni kuiwezesha Serikali kuendesha shughuli zake kwa njia za kitaalamu zaidi na kuhakikisha kuwa kila mwananchi popote alipo anapata huduma au taarifa muhimu zinazotolewa na Serikali kupitia mitandao mbalimbali itakayokuwa karibu naye.
Ameongeza kuwa Mradi huo utaisaidia sana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa na kwa haraka katika kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya kilimwengu kama yanavyoshamiri siku hadi siku duniani.
“Ni jambo la fahari sana kuwa leo hii Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inajiunga rasmi na nchi zingine duniani katika mfumo mpya wa uendeshaji wa shughuli za kiserikali ujulikanao kama E-Government” alisema Shein.
Ameongeza kuwa Mradi huo pia utakuwa ni kichocheo muhimu katika kuendeleza dhamira ya Serikali ya kukuza matumizi ya Teknologia ya habari na Mawasilino nchini.
Amezitaja baadhi ya faida za Serikali Mtandao kuwa ni pamoja na kukuza Elimu katika Skuli za Msingi na Sekondari kwa kupitia Mradi wa T21, ili kukabiliana na mabadiliko yanayoikumba sekta ya habari na mawasiliano.
Aidha Dkt. Shein amefahamisha kuwa Mradi huo pia unaweza kuipunguzia gharama Serikali ya kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu ambapo Madaktari wa ndani wanaweza kuunganishwa na madaktaari waliopo nje ya nchi na kuweza kusaidiana kuwafanyia Operesheni wagonjwa waliopo Zanzibar.
Dkt Shein pia amefahamisha kuwa Mradi huo utatoa fursa nzuri kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini katika kundesha biashara zao ikiwa ni pamoja na kujtangaza,kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri amesema Taasisi za Kiserikali zitaunganishwa katika utendaji na uendeshaji wa shughuli zao kwa njia za uhakika,salama na kwa uharaka.
Aidha amewataka wananchi kuiheshimu miundombinu ya mradi huo ili uweze kuwa endelevu kwa manaufaa ya wananchi wote.
Akitoa salam zake Balozi wa Watu wa China nchini Tanzania Lu Youqing ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano ambayo imekuwa ikitoa kwa nchi ya China katika kuendeleza mahusiano ya nchi husika.
Aidha ameahidi kuzidisha mashirikiano na Zanzibar katika kusaidia wananchi wake kukabiliana na changamoto za maisha hasa katika sekta ya uchumi,elimu na Afya.
Mradi wa Serikali mtandao E-Government ambao umezinduliwa ikiwa ni shamra shamra za Sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar umeigharimu Dola Milion 19 za kimarekani ambazo ni Mkopo nafuu kutoka nchi ya China.
 kwa hisani ya hemed mazrouy kupitia Mzaleno

No comments :

Post a Comment