zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, May 1, 2026

DIASPORA DAY & ZANZIBAR INVESTMENT SUMMIT - 2026!

PPPP
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Dkt. Hussein Ally Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pili la Uwekezaji Zanzibar linalolenga kuvutia wawekezaji wa ndani na wa nje litakalofanyika kuanzia Juni 3 hadi 05 mwaka huu, visiwani Zanzibar. Tarehe 5 Juni, itakuwa ni siku ya Wana-Diaspora (Diaspora Day) katika hili Tamasha na Wana-Diaspora wanaombwa na kitengo cha Diaspora (Ikulu, Zanzibar) kushiriki kikamilifu na kujiandikisha.

Link ya kujiandikisha ni: www.zis.zipa.go.tz


Tamasha hilo linalotarajiwa kuwaleta pamoja washiriki 500 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wawekezaji, watunga sera, wafanyabiashara wakubwa na washirika wa maendeleo linalenga kutanua wigo wa uwekezaji Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hasa atika sekta ya Uchumi wa Buluu.
Akitoa taarifa hiyo Jijini Dar es salaam Waziri wa Kazi na Uwekezaji wa Zanzibar Sharif Ally Sharif amesema kupitia tamasha hilo Serikali imetayarisha miradi ambayo itatoa fursa kwa wawekezaji binafsi kushirikiana na Serikali katika maendeleo ya nchi. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri amesifu ukuaji wa sekta ya Uwekezaji nchini.

No comments :

Post a Comment