NA JOHN NGUNGE
21st January 2013
Mvutano kati ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara na wanasiasa dhidi ya azma ya serikali kusafirisha gesi kutoka mkoani humo hadi Dar es Salaam, inaweza kulikosesha taifa kuitumia gesi hiyo kwa matumizi ya majumbani, magari na viwandani, iwapo bomba la kusafirishia litashindwa kujengwa ndani ya muda uliopangwa.
Kushindwa huko kutafanya hoja waliyokuwa wakitoa awali wawekezaji kwamba gesi hiyo iuzwe nje ya nchi kwa sababu Tanzania hakuna miundombinu ya kuisafirisha kupewa nafasi.
Naibu Waziri wa Nishati, George Simbachawene, alisema jana jijini hapa kuwa mvutano huo usipopatiwa ufumbuzi kabla ya mkandarasi kumaliza kazi yake, wawekezaji watajenga hoja gesi hiyo iuzwe nje ya nchi kwa sababu ya kukosekana kwa miundombinu ya kusafirisha gesi hadi Dar es Salaam.
Aliwaomba wakazi wa Mtwara kuelewa nia nzuri ya serikali ya kutaka kuwaletea maendeleo kwa kukubali bomba hilo la gesi lijengwe.Kushindwa huko kutafanya hoja waliyokuwa wakitoa awali wawekezaji kwamba gesi hiyo iuzwe nje ya nchi kwa sababu Tanzania hakuna miundombinu ya kuisafirisha kupewa nafasi.
Naibu Waziri wa Nishati, George Simbachawene, alisema jana jijini hapa kuwa mvutano huo usipopatiwa ufumbuzi kabla ya mkandarasi kumaliza kazi yake, wawekezaji watajenga hoja gesi hiyo iuzwe nje ya nchi kwa sababu ya kukosekana kwa miundombinu ya kusafirisha gesi hadi Dar es Salaam.
“Tangu awali wawezaji walitaka gesi hiyo iuzwe nje kwa madai kwamba hatuna miundombinu, lakini katika mazungumzo tulifikia makubaliano kwamba lazima isafirishwe hadi Dar es Salaam na tulikubaliana katika kipindi cha miezi minane bomba hilo lazima liwe limekamilika, sasa mvutano huu ukiendelea wawekezaji watajenga hoja yao,” alisema.
Alisema ikifika hatua hiyo taifa litakosa nishati hiyo muhimu kwa matumizi ya majumbani, magari na umeme na akawalaumu baadhi ya wanasiasa kwa kukosa uzalendo katika suala hilo lenye maslahi kwa taifa na sio chama fulani.
“Ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi umepangwa kukamilika katika kipindi cha miezi minane kuanzia sasa, na baada ya hapo hatutakuwa na shida kubwa ya umeme viwandani na kwa matumizi ya majumbani,” alisema.
Alisema serikali itaokoa kiasi cha Sh. trilioni mbili kinachotumika kila mwaka kununulia mafuta.
Akizungumzia faida ambazo wananchi wa Mtwara watakazozipata kwa kusafirisha gesi hiyo ni mapato ya kodi ya asilimia 0.3 ya gesi yote itakayosafirishwa kwa mwaka.
Alisema halmashauri zote za Mtwara zitanufaika na kodi ambayo wataitumia kwa maendeleo ya elimu, afya, maji na miundombinu mbalimbali.
“Pato la asilimia 0.3 ya gesi yote kwa mwaka itaachwa Mtwara, hizo ni fedha nyingi sana, watakuwa wakisoma mita tu na kukata fedha,” alisema.
Alitaka faida nyingine kuwa ujenzi wa kiwanda cha saruji ambacho kitakuwa kikitumia gesi hiyo na hivyo kutoa ajira kwa watu 6,000.
Alisema watajenga mitambo ya kuzalisha na kusindika gesi ambayo itakuwa ikitoa ajira kubwa pamoja na ujenzi wa kiwanda cha mbolea.
“Maeneo yenye ajira kubwa ni hayo kuliko mtambo wa kuzalisha gesi ukijengwa Mtwara…ni gharama kubwa kujenga njia nne za kusafirisha umeme umeme mkubwa wa gesi hadi Dar es Salaam ambako ndiko kwenye soko la nchi na maeneo mengine,” alisema.
Alisema elimu hiyo imetolewa kwa wananchi wa mkoa huo ambapo pia wamewashirikisha tangu mwanzo lakini baadhi ya wanasiasa kwa sababu wanazozijua wameamua kupotosha ukweli huo ikiwa ni ajenda yao katika uchaguzi wa 2015. CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment