NA ROMANA MALLYA
5th January 2013
Mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika, jana amewasilisha kwa Katibu wa Bunge taarifa ya muswada binafsi wa sheria ya kuundwa kwa Baraza la Taifa la Vijana.
Mbunge huyo alisema amelazimika kufikia hatua hiyo, baada ya kupita zaidi ya miaka kumi, na Serikali imekuwa ikiahidi bungeni karibu kila mwaka bila utekelezaji.
Alisema muswada huo wameuwasilisha kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (1) na taarifa ya Muswada huo kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la Mwaka 2007).
Aidha, alisema ameamua kuitekeleza ahadi hiyo kwa kupeleka bungeni muswada binafsi wa kuunda baraza hilo baada ya kuona kimya kwa upande wa serikali.
Aidha, alisema ameamua kuitekeleza ahadi hiyo kwa kupeleka bungeni muswada binafsi wa kuunda baraza hilo baada ya kuona kimya kwa upande wa serikali.
Aliongeza kuwa, katika taarifa hiyo amewasilisha madhumuni, sababu pamoja na nakala ya muswada wenyewe wa sheria ya kuanzisha kwa baraza hilo.
Alisema lengo la kuanzishwa kwa baraza hilo ni ili liweze kuwaratibu vijana nchini katika kutekeleza shughuli zao za kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kimichezo.
Alisema chombo hicho kitawawezesha vijana kuchagiza hali ya utambulisho wa kitaifa wa pamoja na uzalendo na kwamba kimegawanyika katika sehemu nane.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment