Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 20, 2013

Anayetuhumiwa kumgonga trafiki mbaroni

NA MWANDISHI WETU

20th March 2013


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela.
Jeshi la Polisi limemkamata mtuhumiwa anayedaiwa  kumgonga askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, namba P 2492 Elikiza Nko, wakati akiongoza magari eneo la Bamaga jijini Dar es Salaam na kufariki dunia juzi majira ya mchana.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alithibitisha kikosi chake kumkamata mtuhumiwa huyo, Jackson Steven, kwa kushirikiana na  askari polisi Mkoa wa Kinondoni.

Kamanda mpinga alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana baada ya msako mkali ulioongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela.

Alisema mbali na kumkamata mtuhumiwa huyo, alikana kumgonga marehemu kwa kueleza kuwa siku ya tukio hilo gari lake lilikuwa gereji kwa ajili ya matengenezo.

Mpinga alisema baada ya kwenda hadi gereji walilikuta gari hilo na kuamua kulichukua hadi makao makuu ya polisi kwa uchunguzi zaidi.

Marehemu alifariki baada ya kugongwa na gari namba T 328 BML aina ya Landlover Discover na dereva wa gari hilo alikimbia baada ya tukio hilo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment