Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 20, 2013

Mkataba uchimbaji madini

NA MWANDISHI WETU

20th March 2013


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Serikali imesaini mkataba wa miaka 11 na Kampuni ya uchimbaji kutoka nchini Australia, kwa lengo la kuchimba mafuta na gesi katika bonde la Ruhuhu mkoani Ruvuma na Rufiji katika Mkoa wa Pwani.

Akisaini mkataba huo jana Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema serikali imeingia mkataba na Kampuni ya Jacka, baada ya kukubaliana kutimiza masharti yote ya mgawanyo wa mapato.

“Mkataba huu siyo wa siri na wananchi wote watambue hili, kwani tumekuliana na watatimiza yale ambayo serikali tunataka ili tuendeleze uchimbaji, na kama kuna yeyote anataka kufahamu anakaribishwa ofisini,” alisema Muhongo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment