Na Nora Damian, Kelvin Matandiko na Bakari Kihango
Posted Jumatano,Marchi20 2013
Posted Jumatano,Marchi20 2013
KWA UFUPI
Koplo Nko alipatwa na mauti hayo juzi saa 7:00 mchana eneo la Bamaga, baada ya msafara wa Rais Kikwete kupita. Baada ya msafara huo kupita eneo hilo, Koplo Nko aliamua kuingia barabarani kuongoza magari, punde gari aina ya Land Rover
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete jana aliwaongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa Polisi wa Kikosi cha Barabarani, Koplo Elikiza Nko aliyefariki kwa kugongwa na gari iliyovamia msafara wa Rais.
Wakati Rais Kikwete akishiriki tukio hilo, polisi inawashikilia watu wawili kwa mahojiano kuhusuiana na tukio hilo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema watu hao wanahojiwa wapo mikoa tofauti; Dar es Salaam na Arusha.
Mpinga alisema lengo la kuwashikilia watu hao, ni kutaka kuhakikisha wanampata mhusika halisi wa tukio hilo na hatimaye kumfikisha mahakamani.
Koplo Nko anatarajiwa kuzikwa Machi 21, mwaka huu kwenye makaburi ya Bunju A, Manispaa ya Kinondoni.
Jana, Rais Kikwete na viongozi wengine wa Serikali walikwenda kwenda nyumbani kwa marehemu Nko kufariji ndugu wa askari huyo.
Koplo Nko alipatwa na mauti hayo juzi saa 7:00 mchana eneo la Bamaga, baada ya msafara wa Rais Kikwete kupita. Baada ya msafara huo kupita eneo hilo, Koplo Nko aliamua kuingia barabarani kuongoza magari, punde gari aina ya Land Rover ambalo ni mali ya Kanisa la Tanganyika Assemblies of God (TAG) lilichomoka kusikojulikana na kumgonga askari huyo.
Rais Kikwete ambaye akiendelea na ziara yake ya siku mbili.
Awali, akiwa viwanja vya Mnazi Mmoja alisisitiza itolewe adhabu kali kwa wauguzi wanaobainika kughushi vyeti vya taaluma.
Alitoa kauli kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka 60 tangu kuundwa kwa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania, hadi sasa baraza hilo limefanikiwa kuwakamata wauguzi watano waliokutwa na makosa hayo. “Hawa ni watu wa ajabu sana, kama tatizo litakuwa ni sheria basi iongezewe makali,” alisema Rais Kikwete.
No comments :
Post a Comment