Na Raymond Kaminyoge. Mwananchi (email the author)
Posted Alhamisi,Marchi21 2013 saa 14:55 PM
KWA UFUPI
Watu wa mjini tunakula mlo mmoja kwa siku, labda wenzetu wa kipato cha kuaminika wanakula milo yote,” ripoti hiyo inamnukuu mtu mmoja
Inasemekana kuwa hali hiyo haijawahi kutokea tangu nchi ilipopata uhuru wake zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umaskini Tanzania (Repoa) imetoa ripoti ya maoni ya watu ya mwaka 2012 inayoonyesha kwamba maisha ya Watanzania wako katika kipindi kigumu kiuchumi ambacho hakijawahi kutokea tangu kupatikana kwa uhuru hali inayosababisha baadhi yao kupata mlo mmoja kwa siku.

Licha ya ugumu wa maisha, ripoti hiyo inaonyesha kwamba rushwa inazidi kuongezeka katika idara za mahakama, polisi na katika vituo vya afya vya Serikali.
Ripoti hiyo ilisomwa jana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Rose Mwaipopo ambaye alisema utafiti huo uliwahusisha watu 5,136 kutoka katika mikoa 11.
Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Iringa, Arusha, Mbeya, Kigoma, Mwanza Dodoma, Tabora, Mara, Pwani na Kilimanjaro.
Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Iringa, Arusha, Mbeya, Kigoma, Mwanza Dodoma, Tabora, Mara, Pwani na Kilimanjaro.
Ripoti hiyo inawanukuu baadhi ya wananchi wakisema, “ sasa hali ni mbaya kuliko wakati mwingine wowote tuliopata kuushuhudia hapa Tanzania, tunalazimika kula mlo mmoja badala ya mitatu iliyozoeleka.”
Katika ripoti hiyo wananchi wanakiri uchumi kukua ikilinganishwa na siku za nyuma kwa sababu miundombinu kama vile barabara inaonekana lakini maisha ya watu wa kawaida ni magumu ambayo hayajawahi kutokea.
“Watu wa mjini tunakula mlo mmoja kwa siku labda wenzetu wenye kipato cha kuaminika ndiyo wanakula milo yote,” ripoti hiyo inamnukuu mkazi wa Mwananyamala, Dar es Salaam akilalamika.
Katika ripoti hiyo inaonyesha kwamba kuna dhana iliyojengeka katika jamii kwamba wanaofaidi nchi hii kutokana na kukua kwa uchumi na misaada kutoka kwa wahisani ni wanasiasa na watendaji wa Serikali.
Taarifa ya ripoti hiyo inashauri Serikali kufanya kila liwezekanalo ili kutafsiri ukuaji wa uchumi ili uwafikie wananchi.
Aidha, ripoti hiyo inasema Serikali inatakiwa kupunguza mfumko wa bei na kwamba licha ya kuwa unasababishwa na bidhaa za kutoka nje lakini unaweza kupunguzwa kwa matumizi yasiyo ya lazima
.
.
No comments :
Post a Comment