Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, March 18, 2013

Makachero FBI kazi yaiva kuwasaka wauaji wa Padri Z’bar

FBI in action in the States!
NA MWINYI SADALLAH
18th March 2013
Msako wa kuwatafuta watu wanaofanya hujuma dhidi ya viongozi wa dini umechukua sura mpya Zanzibar baada ya taarifa za mitandao ya simu kuanzia kufanyiwa uchunguzi na maofisa wa upelelezi wa jeshi la polisi visiwani humo.
Hii inakuja wiki chache baada ya makachero hao kutoa picha ya mtu anayedhaniwa kuhusika kumuua Padri Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoliki Februari 17, mwaka huu visiwani humo.
Msako huo unawahusisha wapelelezi wa ndani wanaoshirikiana na makachero wa FBI kutafuta namba za simu zinazotumiwa na watu hao hasa katika siku ya tukio la kupigwa risasi kwa Padri Mushi eneo la Beit el Ras.
Taarifa za uchunguzi zilizoifikia NIPASHE zinasema kwamba mitandao yote ya kampuni za simu iliyotumika kufanya mawasiliano katika eneo la tukio, imeanza kufanyiwa uchunguzi na makachero wa FBI wanaoshirikiana na timu maalum ya wapelelezi wa ndani.
Ofisa mmoja wa kampuni ya simu ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema maofisa hao wa upelelezi wametaka wachapishiwe taarifa za namba zote zilizofanya mawasiliano kuanzia saa 12:00 hadi saa 1:00 asubuhi mara baada ya tukio.
Ofisa huyo alisema kampuni yao tayari imekwishatii na kutekeleza maelekezo hayo kwa lengo la kusaidia kufanikisha uchunguzi wa watu waliomuua kwa kumpiga risasi Padri Mushi, Februari, mwaka huu.
Hata hivyo, Kamishana wa Polisi Zanzibar, Musal Ali Mussa, kuhusu suala la pekuapekua ya makachero katika mitandao ya simu alisema uchunguzi haujasimama, haujasita ila unaendelea katika kila hatua itakayofaa.
“Uchunguzi unaendelea, haujasimama, tumefikia hatua kubwa ila tunahitaji ushirikiano zaidi kutoka kwa wasamaria wema kufanikisha jambo hili na mengine,” alisema Kamishna Mussa.
Aliongeza: “Jeshi la Polisi lina matumaini makubwa ya kuwatia mikononi watu hao, iko siku watafikishwa mbele ya mikono ya sheria, kuna watu tunawahoji katika hatua za awali za uchunguzi.”
Alisema licha ya mchoro wa picha ya mtu anayedaiwa kuhusika  kumpiga risasi Padri  Mushi, tayari mchoro huo umesambazwa katika maeneo mbalimbali kama juhudi za polisi kumtafuta na kumkamata.
Viongozi watatu wa kidini hadi sasa wamehujumiwa kufuatia vitendo hivyo akiwamo Katibu wa Mufti Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga, ambaye alimwagiwa tindikali usoni, Padri Ambrose Mkenda, kujeruhiwa kwa risasi na Padri Mushi, aliyeuawa na kuzikwa Kitope mwaka huu.
Padri Mushi, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph- Shangani Mjini Magharibi, visiwani Zanzibar, aliuawa kikatili Februari 17, mwaka huu kwa kupigwa risasi tatu kichwani huku wauaji wake wakitoroka bila kukamatwa.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment