Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, March 18, 2013

Polisi wakamata ‘unga’ Zanzibar

NA MWINYI SADALLAH
18th March 2013
Kilo tano za dawa za kulevya zimekamatwa katika uwanja wa kimataifa wa Abeid Amani Karume jana jioni zikisafirishwa kutoka Zanzibar kwenda nchini Italia.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema dawa hizo zina thamani ya Sh. milioni 200 na kwamba mtu mmoja anashikiliwa kwa kuhusika na tukio hilo.
Alimtaja mtu huyo kuwa ni Alex Vasileios Nitis (24) raia wa Ugiriki ingawa mama yake ni Mtanzania na kwamba alikuwa anasafiri na shirika la ndege la Kenya.
Kamishna Mussa alisema dawa hizo zilihifadhiwa katika mfuko wa rangi ya hudhurungi na kuwekwa chini ya begi ukiwa umebandikwa kwa kutumia gundi na kufunikwa kwa mfuko maalum wa begi hilo.
Alisema raia huyo wa Ugiriki alikuwa na hati ya kusafiria yenye No A 13424772 iliyotolewa Juni 15 mwaka 2012, ni mkazi wa mji mkuu wa Ugiriki, Ethens.
Akifafanua alisema mtuhumiwa alikamatwa akiwa tayari kwenye chumba cha kusafiria mnamo majira ya saa 12.15 jioni.
Polisi pia walimkamata mtuhumiwa huyo akiwa na simu mbili ambazo alisema huenda zikasaidia kuufahamu mtandao wa uingizaji na usafirishaji wa dawa hizi nchini.
Kuanzia Januari mwaka jana hadi Machi mwaka huu tayari watu sita wamekamatwa na dawa za kulevya ambapo watatu ni katika uwanja wa ndege wa kimataifa na wengine watatu katika bandari ya Malindi mjini Unguja.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment