Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 26, 2013

Viongozi wa kiislamu bado wateseka ndani – Kesi ya UAMSHO

Written by   //  25/03/2013

uamsho
Salma Said,
  • Haieleweki ni vipi viongozi hao wanashikiliwa huku upelelezi au uchunguzi ukiwa haujakamilika.
KESI ya jinai inayowakabili viongozi wa Dini wa Jumuiya ya Uwamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) imeanza kusomwa upya leo katika Mahakama Kuu ya Zanzibar baada ya maamuzi ya awali kutenguliwa.
Kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2012 ilisomwa mbele ya Jaji Fatma Hamid Mahmoud na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ramadhan Nassib, ambae aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni,Msellem Ali Mselem (52) mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47) mkaazi wa Makadara na Azzan Khalid Hamdan (48) mkaazi wa Mfenesini mkoa wa Mjini wa Magharibi Unguja.
Wengine ni Suleiman Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakari Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe na Abdallah Said (48) mkaazi wa Misufini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Washitakiwa wote kwa pamoja walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kuharibu mali, Uchochezi, Ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula njama ya kufanya kosa huku kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne Azan Khalid ambae anadaiwa kufanya vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa Amani.
Makosa yote hayo yandaiawa kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 katika maeneo tofauti ambapo washitakiwa hao walipotakiwa kujibu tuhuma zao walizikana.
Mara baada ya kuwasomea mashitaka hayo, Mwenesha Mashtaka wa Serikali,. Nassib alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo tayari umeshakamilika lakini hata hivyo aliiomba mahakama hiyo kufanya subra ya kuweza kuamuwa maamuzi yoyote kutokana na upande huo wa mashtaka kukata rufaa kitendo ambacho alisema kwamba iwapo mahakama hiyo itaendelea na kesi hiyo kunaweza mahakama ya rufaa ikatoa maamuzi ambayo yataweza kuathiri maamuzi ya mahakama hiyo.
Kwa upande wa mawakili wa watetezi uliokuwa ukiongozwa na Salim Toufiq, Abdallah Juma na Suleiman Abdallah, uliiomba mahakama hiyo kuwapatia dhamana washitakiwa wake hao hasa ikiangaliwa kuwa tayari washitakiwa hao wameshakaa ndani kwa muda
mrefu.
“Mheshimiwa Jaji tumefurahi kuona kwamba kwa mara ya kwanza upande wa mashtaka unatamka kuwa upelelezi umekamilika lakini isiwe sababu ya kuendelea kubakia rumande wateja wetu kwa vile muda wa kukaa kwako umekuwa mwingi na kupelekea haki yao ya msingi ya dhamana kunyimwa”,
alisema. Toufiq
Hata hivyo Jaji Fatma alisema kuwa atayachukuwa maombi ya pande yote mbili na kuyapitia kwa umakini ili baadae aweze kutoa maamuzi yaliyo sahihi kutokana na kuwa ni mgeni wa kesi hiyo na jalada lake amelipokea kwa muda mchache ambao haukupata nafasi ya kuipitia vizuri.
“Nayachukuwa maombi yote mawili nitayatafakari kwa kina na kuja kutoa uamuzi unaofaa”,
alisema Jaji huyo ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Mahakama hiyo aliyemaliza muda wake wa kustaafu mwaka jana.
Katika maamuzi ya Jaji Abraham Mwampashi alisema kesi hiyo inapaswa kuanza kupaya kutokana na kuwa mrajis hana mamlaka na pia kupinga maamuzi ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kuwanyima dhamana wahutumiwa hao ambao wanakabiliwa na makosa mbali mbali ikiwemo kuhatarisha usalama wa nchi na kuharibu mali za watu binafsi na serikali, hata hivyo serikali ilikata rufaa kupinga maamuzi ya Jaji Mwampashi na kupangiwa jaji Fatma, kesi hiyo ameakhirishwa hadi Machi 27 mwaka huu, .


No comments :

Post a Comment