Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 25, 2013

Maalim aonya wanaouza miche ya karafuu nje

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

 Jumatano,Aprili24  2013
KWA UFUPI


Alisema tabia ya kukata miti kiholela ni hatari kwa mazingira na husababisha athari kubwa kiuchumi, lakini vitendo vya kusafirisha nje ya nchi miche ya mikarafuu kinaweza kushusha hadhi ya Zanzibar iliyojijengea kwa miaka mingi kuwa mzalishaji mkuu wa karafuu.
Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad ameonya kuwa Serikali haitavumilia na itawachukulia hatua za kisheria watu watakaobainika kukata miti na kusafirisha miche ya miti ya mikarafuu nje ya nchi kinyume cha sheria.
Maalim Seif alitoa onyo hilo Bwagamoyo Mtambwe, Mkoa wa Kaskazini Pemba, alipokuwa akizindua kampeni ya upandaji miti Zanzibar.
Alisema baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kukata miti ovyo, ikiwamo mikarafuu na wapo ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kuisafirisha miche ya mikarafuu nje ya nchi, ikiwamo Kenya.
Alisema tabia ya kukata miti kiholela ni hatari kwa mazingira na husababisha athari kubwa kiuchumi, lakini vitendo vya kusafirisha nje ya nchi miche ya mikarafuu kinaweza kushusha hadhi ya Zanzibar iliyojijengea kwa miaka mingi kuwa mzalishaji mkuu wa karafuu.
Alieleza kuwa karafuu ni alama ya Zanzibar, ambayo imeifanya ijuilikane duniani kote kuwa ni visiwa vya viungo, lakini baada ya watu kuona thamani ya zao hilo ilishuka katika miaka iliyopita walilidharau na kuikata miti hiyo kwa ajili ya kujengea nyumba, kuni na makaa.
Alisema katika karne iliyopita zao la karafuu lilithaminiwa sana na wazee waliliotesha kwa wingi hadi kufikia hatua Zanzibar ikizalisha tani zaidi ya 35, 000
.

1 comment :

  1. Athari kubwa katika kisiwa cha Pemba tayari inaonekana kutokana na ukataji wa miti ovyo ovyo.Kiasi miaka 15 nyuma ilikuwa unapo safiri kutoka pembe hadi pembe ya kisiwa,ilkuwa ni shida kushuhudia mabonde njiani kwa vile miti,na hasa mikarafuu,ilkuwa imetanda na kushikamana.Fanya safari ya aina hiyo leo na utajionea mabonde bila ya usumbufu.Si hayo tuu,la kusikitisha zaidi ni utoweko wa aina ya miti ya matunda ADIMU kama FUU,CHOCHA,VITORIRO,MBURA,ZAMBARAU na mengi.Tatizo ni Viongozi wa serikali hawajali maslah ya kisiwa ila Matumbo yao.

    ReplyDelete