24/4/2013
ZanzibariYetu
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hatua ya Ubalozi wa Marekani nchini kumtunuku tunzo ya Mwanamke Jasiri, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej kimekipa heshima kubwa chama hicho na kinamaanisha uwezo mkubwa walio nao wanawake kiutendaji.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hatua ya Ubalozi wa Marekani nchini kumtunuku tunzo ya Mwanamke Jasiri, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej kimekipa heshima kubwa chama hicho na kinamaanisha uwezo mkubwa walio nao wanawake kiutendaji.
Maalim Seif amesema hayo jana huko hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar alipokuwa akihutubia kwenye sherehe maalum zilizoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa CUF kumpongeza Waziri Ferej kwa kupewa tunzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania 2013, iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani mapema mwezi huu.
Amesema Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania haukufanya upendeleo na wala haujakosea kumpa tunzo Waziri Ferej kwa vile anastahiki, kwa sababu ni mchapa kazi hodari aliyejitokeza na kujipambanua na wengine.
“Mimi nimebahatika kufanya kazi na Waziri Fatma Ferej, na hivi sasa ni Waziri katika Ofisi yangu, kazi anazifanya vizuri na anahakikisha ameifuatilia mpaka ifike mwisho. Kwa kweli Ubalozi wa Marekani haujakosea kumteua na kumpa tunzo hiyo”, alisema Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
ewataka wanawake katika chama cha CUF kuhakikisha wanazidisha ari ya utekelezaji wa majukumu yao na kuonesha uwezo mkubwa zaidi, ili kuzidi kuithibitishia Dunia na jamii kuwa wanawake wanau uwezo mkubwa wa kiutendaji na kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Nae, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia katika sherehe hizo aliwaasa wanaume kujiepusha na tabia ya kuwaonea wivu wake zao wanapokuwa wakijishughulisha na harakati za kimaendeleo, ili waweze kutoa mchango wao katika kuendeleza mbele maendeleo yao na jamii nzima.
Alieleza kuwa tabia ya ubaguzi katika kuwapatia elimu watoto wakike na wa kiumehe, kwa sababu elimu ndiyo itakayowawezesha kujijengea uwezo na kuzitumia fursa za kujiendeleza kiuchumi na kimaendeleo.
Mapema katika risala yao iliyosomwa na Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake CUF, Zahra Ali Hamad, wana jumuiya hiyo walisema Waziri Fatma anastahiki na kuna kila sababu ya kutunukiwa tunzo hiyo.
“Waziri Fatma ameonesha wazi kuwa ni kiongozi aliyejitolea kwa chama chake na Serikali. Hii inathibitisha kwamba sisi wanawake tunapopewa nafasi tuna uwezo wa kuisaidia jamii katika masuala muhimu na mazito sawa au zaidi ya wanaume”, walisema katika risala yao.
Waliahidi kushirikiana naye katika kukitumikia chama cha CUF, na wamemuomba atumie uwezo wake na ujasiri alionao kuwasaidia wanawake wengine, ili waweze kujijengea uwezo wa kutumikia jamii kwa ufanisi mkubwa.
Khamis Haji, OMKR
No comments :
Post a Comment