NA MWINYI SADALLAH
11th April 2013
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amezindua njia mpya ya umeme na kuutaka uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), kudhibiti mianya ya ubadhirifu ili wananchi waweze kupata huduma bora ya nishati visiwani humo.
Akiwahutubia maelfu ya wananchi katika kilele cha kuzindua njia mpya ya umeme iliyofanyika katika uwanja wa Amaan mjini hapa jana, Dk. Shein alisema tangu mwaka 2009 wananchi wamekuwa hawana huduma ya umeme wa uhakika visiwani humo.
Alisema kukamilika kwa mradi huo kumeleta faraja kwa serikali, wawekezaji na wananchi, kwa vile utasaidia kufikia lengo la kupunguza umaskini na kuongeza uchumi kwa wananchi.
“Shukran za pekee ziwaendee wananchi wa Marekani kwa msaada mkubwa waliotupatia ambao umeondoa tatizo la mgao wa umeme uliokuwa ukirudisha nyuma maendeleo yetu” alisema Dk. Shein.
Alisema serikali ina matumaini makubwa kuwa njia hiyo mpya ya umeme yenye uwezo wa megawati 100, itasaidia kuongeza kasi ya uwekezaji katika sekta ya utalii na viwanda katika uzalishaji wa ndani na nje ya Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

No comments :
Post a Comment