Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, April 28, 2013

Wananchi wanasemaje kuhusu muungano?

Na Fidelis Butahe

 Aprili27  2013
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzishwa Aprili 26 mwaka 1964, baada ya Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja) kuungana.
Nchi hizi mbili ziliungana baada ya Tanganyika kupata uhuru wake Desemba 9 mwaka 1961 kutoka kwa Waingereza na Zanzibar kupata uhuru Januari 12 mwaka 1964, baada ya kumwondoa kwa nguvu Sultan.
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, hayati Sheikh Abeid Aman Karume Aprili 22 mwaka 1964 mjini Zanzibar.
Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar Aprili 26 mwaka 1964 na Aprili 27 mwaka 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam na kubadilishana hati za Muungano.
Baada ya kuungana, jina lililotambulika ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Hata hivyo, jina hilo lilibadilishwa baadaye Oktoba 28 mwaka 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.
Tangu pande hizo mbili kuungana, juzi ndiyo ulikuwa mwaka wa 49 ambapo pamoja na mambo mengine, bado kuna kero na hoja za watu mbalimbali juu ya muungano huo, kwani wapo wanaotaka uvunjike na wapo wanaotaka uendelee.
Yafuatayo ni maoni ya baadhi ya wananchi wa Dar es Salaam kuhusu muungano.
Michael James (39), mkazi wa Tabata Kimanga, “Nataka muungano uendelee kwa sababu ni miaka 49 tangu tuungane, hivyo tukitengana tutarudi nyuma kimaendeleo kwa kuwa tumeshakuwa kitu kimoja.
Kikubwa kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo walau itatoa jibu ya kero za muungano.
Iman Mohammed Saleh (23), mkazi wa Matumbi, anasema vurugu zinazodaiwa kuwa za kidini zilizosababisha makanisa kuchomwa moto na watu kadhaa kuuawa huko Zanzibar isiwe sababu ya kuutizama muungano kwa jicho baya.
Anasema kuna nchi zilizopiga hatua kubwa baada ya kuungana au kuamua kushirikiana, naamini kuwa muungano wetu tukiudumisha tutapata faida kubwa.
Edmund Mganda (55) wa Gongo la Mboto, anasema wakati pande hizi mbili zinaungana nakumbuka hali ilivyokuwa licha ya kuwa nilikuwa kijana mdogo, waliotuunganisha wametangulia mbele za haki, walikuwa na maana kubwa kuamua kuungana hivyo nasi hatutakiwi kuvunja muungano.
Siku zote umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu, kama kuna kasoro zijadiliwe na kuja na ufumbuzi wa kudumu.
Aboubakar Hassan (42), wa Mbagala Rangi Tatu, anasema muungano huu ndiyo uliofikisha Tanzania hapa ilipo, pengine tusingeungana nchi yetu isingekuwa na amani kama ilivyo sasa. Hata tukiamua kutengana tutajikuta tunapigana na kubaguana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu tayari tumetengeneza undugu mpaka kufikia hatua ya kuoleana.
Madofe Ngoma (31), mkazi wa Ubungo, anasema muungano ni ushirikiano, undugu na umoja, kati ya mambo hayo matatu moja likitoweka ni wazi kuwa nchi yetu itayumba.
Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, huwezi kuacha, kikubwa ni kuwasisitiza wanasiasa wetu kutenganisha siasa na masuala ya muungano kwani haviendi pamoja.
Robert Venance (21), wa Kimara
anasema ingawa hafaidiki kabisa na muungano, lakini hataki kabisa uvunjike kwa sababu hakuna sababu za msingi.
“Kama tuliungana miaka 49 iliyopita iweje tutengane kwa siku moja tu, tena bila sababu za msingi,” anasisitiza.
Jane Patrick (32), mkazi wa Manzese, anasema “Binafsi nataka muungano uvunjike kwa kuwa watu kutoka bara tukienda Zanzibar tunabaguliwa sana. Hasa ukiwa mfanyabiashara ndio zaidi, watakubagua na kukutenga lakini wao wakija bara wanafanya shughuli zao kwa raha na amani kubwa.
Lwembu Henjewele (43),mkazi wa Kimara anataka muungano uendelee kwa kuwa una maana kubwa kwa nchi yetu,
“Maendeleo na amani tuliyonayo inatokana na kuwepo kwa muungano huu,” ananena.
Anasema licha ya kuwa ndugu, pia kila upande unautegemea upande mwingine katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi, hivyo kutengana ni sawa na kujichimbia kaburi sisi wenyewe.
Lilian Andrew (25), wa Kinondoni anasema “Mpaka tulipofikia hatua ya kuungana ni wazi kuwa tulikubaliana katika masuala ya msingi sasa iweje leo tuvunje muungano, iwe hivyo kwa maslahi ya nani.
“Binafsi naona muungano huu una manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania, kasoro zilizopo tuzimalize katika meza ya majadiliano,” anasema.
Kayanda Tumbo (30), wa Vingunguti, anasema “Muungano uendelee, ila tatizo kubwa ninaloliona kwa sasa ni kuwepo kwa vuguvugu la kidini ambalo kwa kiasi kikubwa linatumika kuhatarisha muungano wetu.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar zinatakiwa kukaa na kutatua kero mbalimbali za muungano likiwemo hili na udini, ubinafsi na ubaguzi.
Ina Mohammed (25), wa Mwananyamala anasema “Kwa miaka 50 sasa nchi yetu imekuwa na amani ambayo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na muungano imara. Wapo wanaotaka muungano uvunjike lakini wanataka hivyo kwa kuwa bado haujavunjika, siku ukivunjika ndio watajua umuhimu wake.
Shakila Iddi (21) wa Kaweanasema “Kuna baadhi ya nchi barani Afrika zimeingia katika machafuko kwa sababu tu ya wananchi wake kutokuwa tayari kushirikiana, kuungana na kuwa kitu kimoja.
Muungano kati yetu na Zanzibar unatakiwa kudumishwa na kuenziwa kwa kuwa una maana kubwa na pia ni mfano kwa nchi nyingine duniani.
Chanzo:Mwananchi

No comments :

Post a Comment