Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 29, 2013

ZRB: Precision Air inatuchezea

Written by   //  29/04/2013  

ZRB: Precision Air inatuchezea
Na Mwandishi wetu
KAMISHNA wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Abdi Khamis Faki ameelezea kusikitishwa na kitendo cha Shirika la Ndege la Precision Air kushindwa kulipa kodi inayodaiwa na bodi hiyo.
Kamishna Abdi alisema shirika hilo ‘linawachezea’ kwa kuwa mashirika yote ya ndege yanayotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar, yamekuwa yakilipa kodi.
Akizungumza kwa njia ya simu na Zanzibar Leo jana, alisema kitendo cha kampuni hiyo kutolipa kodi kunainyima serikali mapato yake.
Shirika hilo tayari limezuiwa kutoa huduma Zanzibar kutokana na kudaiwa mamilioni ya fedha na bodi hiyo.
“Precision wanatuchezea, wao ni nani? Kwanini makampuni mengine yanalipa kodi zao,” alihoji.
Zanzibar Leo lilipotaka ufafanuzi kama shirika hilo limeshalipa deni lake baada ya kupelekewa barua ya kusitishwa kutoa huduma Zanzibar, Kamishna Abdi alisema limelipa shilingi milioni 50 pamoja na kuahidi wiki iliyopita kulipa dola za Marekani 20,000.
Hata hivyo, alisema watafuatilia Jumatatu (leo) kufahamu kama wamelipa dola hizo au laa.
Barua ya Aprili 25 ya ZRB iliyosainiwa na Kamisha huyo, imelifungia shirika hilo kutoa huduma Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 43(1) cha sheria ya usimamizi wa kodi namba saba ya mwaka 2009.
Barua hiyo yenye kumbukumbu namba ZRBA.2/VOL.1/139, inasema hatua hiyo imeanza Aprili 25 mwaka huu hadi hapo shirika hilo litakapolipa deni lote linalodaiwa na ZRB.
Shirika hilo linadaiwa gharama za huduma na ada ya usalama kwa miezi ya Januari,Februari na Machi 2013 inayofikia dola za Marekani 347,066 na shilingi milioni 144.818.
Pia inadaiwa fedha za adhabu kwa kuchelewesha malipo kwa miezi ya Februari hadi Agosti 2012 yanayofikia dola za Marekani 1,644,725 na shilingi milioni 70,479,200.
Kwa mujibu wa barua hiyo, Precision Air imeshindwa kulipa licha ya ZRB kuchukua hatua za kuwakumbusha.
Gazeti hili lilipotembelea ofisi za shirika hilo zilizopo uwanja wa ndege wa Zanzibar, halikukutia abiria yeyote anaesafiri kwa shirika hilo na kuambiwa kuwa huduma zimefungwa.
Afisa wa Precision Air tawi la Zanzibar, ambae hakutaka jina lake litajwe alisema kwa sasa huduma za shirika hilo zimefungwa na hakuna ndege ya shirika hilo inayoruka au kutua katika uwanja huo.
Hata hivyo, alisema hawezi kuzungumzia kama shirika lake limeshalipa deni hilo kwa madai kuwa yeye si msemaji wa shirika akimuelekeza mwandishi wetu kufunga safari hadi Dar es Salaam kwenda kuonana na watendaji wakuu.
Nakala ya barua ya ZRB ya kuchukua hatua ya kufunga huduma za shirika hilo Zanzibar pia imetumwa kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano Zanzibar, Naibu Kamishna wa TRA-Zanzibar, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, Meneja wa Precision Air tawi la Zanzibar, Kamishna wa polisi Zanzibar na Mkuu wa polisi katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Chanzo: Zanzinews

3 comments :

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  3. Naona tunajichezea wenyewe! Hebu oneni kwa wenzetu kwenye sheria kama Corporation linaweza kukaa na kodi ya serikali kiasi hichi cha muda kama wanavyofanya hawa jamaa wa Precision. Hii yote ni kuwa hapa petu hapana sheria isipokuwa pata mpatae tu basi!

    "Beware tax penalties from the CRA
    By Dale Jackson | Pay Day – 2 hours 33 minutes ago
    17

    The Canadian Press - The Canada Revenue Agency headquarters in Ottawa is shown on Friday, November 4, 2011. THE CANADIAN PRESS/Sean Kilpatrick
    We like to think of Canada as a gentle, compassionate nation. Think again.
    When it comes to collecting taxes the Canada Revenue Agency has the full force of the law at its disposal.
    If the CRA owes you money this tax season, relax. It’s in no hurry to pay you. But if you owe on income generated during the 2012 calendar year - even if you are self employed - the deadline to pay up is April 30.
    If you miss the deadline, the clock is ticking and the costs could be mounting.
    Late filing penalty
    Starting May 1st any amount owing is subject to a late-filing penalty of 5 per cent compounded daily, plus 1 per cent for each full month that the return is late, to a maximum of 12 months.
    After a year it’s no more Mr. Nice Guy. The CRA reserves the right to boost the late-filing penalty to 10 per cent of the balance owing plus 2 per cent for each full month you're late, up to 20 months.
    Those penalties don’t include any amount over what you think you owe. In other words, if you miscalculate taxes owning in your favour and they find out you actually owe more, the late-filing penalty applies to their assessment.
    The penalties also apply to overdue Canada/Quebec Pension Plan contributions and Employment Insurance premiums.
    The CRA will keep you informed of your status through the mail.
    Tell no lies
    If you make a false statement, and the CRA believes you knowingly falsified your tax return, the penalty is $100 or 50 per cent of the falsified amount, whichever is higher.
    Any omissions that the CRA believes were made intentionally are subject to the same penalty.
    The taxman isn’t void of forgiveness though. The penalty could be waived under the Voluntary Disclosures Program if you ‘fess up before your false statement or omission is discovered.
    The CRA’s double standard
    You might notice the interest rates charged by the CRA on taxes owing are much higher than the rates paid on comparative government bonds, which are mostly below 2 per cent.
    To make matter worse, the rate the CRA charges is subject to change every three months and it will likely rise as interest rates climb in the broader economy.
    Don’t expect the same generous rates if the CRA owes you money. The CRA pays no interest on regular payroll deductions throughout the year to the time you receive a refund in the spring.
    Individuals who are owed money due to an overpayment are given 3 per cent and money owed to corporations generates a 1-per-cent return.
    One interesting side note that could help explain the CRA’s double standard is the reported propensity for clever corporate accountants to intentionally over pay. A risk-free pay back rate of 5 per cent handily beats any return from the bond market. Nice try, though.
    Compassion
    On a serious note, many livelihoods have been left in shambles by life-long entanglements between individuals and the CRA. It normally begins with simply neglecting to file in any given year and compounds to the point where the individual is drowning in taxes-owing statements and legal threats.
    Individuals live and die but the CRA trudges on as an institution with the backing of a legal system that can impose liens on property, and even incarceration.
    The CRA’s ultimate goal is to get its money and is not entirely without compassion. Taxpayer relief provisions are provided for individuals who are victims of circumstances beyond their control.
    Tax professionals can help broker a satisfactory arrangement but it’s important to get qualified advice before things spin out of control."

    ReplyDelete