Written by Ashakh (Kiongozi) // 03/05/2013
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Maendeleo ya haraka yanaweza kupatikana kwa Mataifa Machanga iwapo suala la matumizi ya Mtandao wa kisasa wa Mawasiliano ya Kiteknolojia utapewa msukumo unaostahiki.
Alisema mfumo huo wa Teknolojia unaweza pia kutoa ajira hapo baadaye kwa kuangalia zaidi maeneo ya Vijijini ambayo huduma hizo za mawasiliano hazijafika na mwengine ziko katika kiango hafifu.
Balozi Seif alisema hayo wakati akiifungua warsha ya siku tano kuhusu mawasiliano Vijijini iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote wenye makao makuu yake Nchini Uholanzi, warsha ambayo inafanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Kimataifa ya Melia iliyopo Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema Kilimo, Biashara na hata Elimu ni sekta za msingi zinazoweza kuendelezwa kwa kutumia mfumo huo wa Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano.Balozi Seif alifahamisha kwamba Serkali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeanza hatua za kufuata mfumo huu ili kutengeneza mazingira bora yatakayowezesha kukuza chumi wa Taifa katika kutumia Taaluma hiyo.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea hafaja yake kutokana na warsha hiyo kufanyika Nchini Tanzania, fursaambayo itasaidia kuunganisha nguvu za pamoja katika kukabiliana na changamoto zilizomo kwenye mfumo huo wa mawasiliano.“ Tumeshuhudia Mataifa kama vile Chile, Uturuki na Malaysia yalivyopiga hatua kubwa na ya haraka katika kuimarisha uchumi wao baada ya kuamua kutumia mfumo huo wa mawasiliano “.
Alisisitiza Balozi Seif.Aliwataka washiriki wa warsha hiyo ya mfuko wa mawasiliano kwa wote kufikiria njia zitakazowezesha mawasiliano ya teknolojia ya kisasa kuwafikia wananachi hasa wale walioko Vijijini wakati watakaporejea katika Mataifa yao.Aliongeza kwamba licha ya Zanzibar kusifiwa kwa kupiga hatua kubwa ya mawasiliano lakini bado Serikali inaendelea na mikakati ya kusimamia upatikanaji wa huduma za mawasiliano ili ziwafikie wananchi wote mijini na Vijijini.Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Florens Martin Turuka alisema lengo la warsha hiyo ni kujenga nguvu zitakazosaidia kufikisha mawasiliano sehemu zisizo na huduma hizo.Dr. Turuka alifahamisha kwamba mfumo huu mpya ambao unaanza kuelekezwa katika mataifa machanga unakusudiwa kuanzisha mpango maalum wa mafunzo ya maskuli kwa kutumia mtandao wa moja kwa moja wa mawasiliano kati ya sehemu moja hadi nyengine.Alisema hatua hiyo itakwenda sambamba na huduma za mawailiano ambazo zitawahusisha baadhi ya wasimamizi waliojiandaa kutoka huduma hizo kwa kupatiwa ruzuku katika maeneo ya vijijini.“ Tumefarajika kuona wataalamu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote wameamua kuifanya warsha hii hapa Zanzibar kufuatia Visiwa hivi kupiga hatua ya maendeleo katika matumizi ya mawasiliano ya simu za mkononi “ . Alisisitiza Dr. Turuka.Warsha hii ya sita ya mawasiliano imeshirikisha Mataifa 12 ya Bara la Afrika wakiwemo pia wawakilishi wa mataifa ya India, Malaysia na Marekani wakiwa chini ya udhamini wa Mfuko wa mawasiliano kwa wote kutoka Nchini Uholanzi.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment