Written by Ashakh (Kiongozi) // 02/05/2013
Na Masoud Ali
2-5-2013
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF ambae pia ni Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif hamad amewashukuru wananchi kisiwani Pemba kwa kujitokeza kwa wingi na kuwa wastaarabu katika uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya katiba uliofanyika hivi karibuni wenye lengo la kuunda katiba mpya Tanzania.
Ameyasema hayo huko Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ghafla maalumu ya kukabidhi vifaa mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni 42, miongoni mwa vifaa hivo ni pamoja na Pikipiki(2),baiskeli(58)jezi set(27),mipira(135),na tv flat(11) kwa wananchi wa jimbo hilo vilivotolewa na Mbunge wao Khatib Said(Obama) huko konde mkoa wa kaskazini Pemba.
Pia Maalim Seif amewataka wana CUF wa Jimbo hilo kuvithamini vifaa hivyo vilivotolewa na mbunge wao kwa lengo la kuleta maendeleo zaidi jimboni humo.
Aidha katibu mkuu huyo amewaasa wananchi kisiwani humo na wazanzibar kwa ujumla kuwa na subra huku wakisubiri kwa hamu kubwa sana rasimu ya awali ya katiba itakayotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba mpya hivi karibuni.
Wakati akiwashajihisha wananchi kuitetea Zanzibar yenye mamalaka kamili Maalim Seif alionyesha miongoni mwa kasoro ziliomo ndani ya muungangao ambazo amezishuhudia wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika hivi karibuni.
Akibainisha miongoni mwa kero hizo ni hile ya kutokuwepo kwa bedera ya Rais wa Zanzibar kwenye sherehe hizo na badala yake kulikuwa na bendera ya Muungano,bendera ya Rais Kikwete,pamoja na bendera ya mkuu wa Jeshi Tanzania, huku mlingoti wa bendera ya Rais wa Zanzibar ukiwa mtupu bila ya bendera wakati Rais alikuwepo kwenye sherehe hizo.
Maalim Seif pamoja na baadhi ya wajumbe wengine akiwemo Mkurugenzi wa habari uenezi na mawasiliano ya Umma Mh,Salim Biman watarejea Unguja hapo keho mnamo majira ya alasiri baada ya kumaliza rasmi ziara ya siku moja kisiwani humo.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment