NA JOHN NGUNGE
16th June 2013
Mkutano huo ulifanyika katika viwanja vya Soweto vilivyopo katika kata hiyo na wakati Mbowe akiwa anakaribia kumaliza kufunga kampeni zake, na huku wanachama wakijiandaa kufanya harambee, mtu mmoja ambaye hajafahamika anadaikuwa kurusha bomu kwenye mkusanyiko wa mkutano huo na taarifa za awali zilidai kuwa watu watatu walifariki kutokana na mlipuko huo.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema jana kuwa kulitokea mlipuko wa kitu kama bomu lililorushwa na mtu ambaye bado hajafahamika ni nani.
Kufuatia mlipuko huo, polisi waliokuwa wakifanya ulinzi katika mkutano huo, walilipua risasi za moto na inadaiwa kuwa zaidi ya watu 6O hadi 70 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali za Selian na ya Mount Meru.
Tukio hilo limekuja huku maelfu ya wanachama leo wa vyama vya siasa wakipiga kura kuwachagua madiwani wa kata za Kaloleni, Elerai, Kimandolu na Themi.
Hadi NIPASHE JUMAPILI inakwenda mitamboni, Mbowe na viongozi wa mkoa walikuwa wameelekea Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kuwajulia hali watu walioathirika na bomu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas, alikuja eneo la tukio lakini hakutaka kuzungumza lolote kuhusu kuhusu mlipuko huo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment