dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 23, 2013

CUF kuandamana Jumamosi kwenda Ikulu

23rd June 2013
Chama cha Wananchi (CUF), kimeandaa maandamano ya amani Jumamosi ijayo kuelekea Ikulu kwa lengo la kumfikishia malalamiko Rais Jakaya Kikwete, kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanywa na jeshi la polisi na JWTZ huko Mtwara.
Pia maandamano hayo yamelenga kumtaka Rais kuhakikisha kuwa ripoti ya uchunguzi ya maafa ya mlipuko wa bomu kule Arusha inawekwa wazi na wahusika wote wanachukuliwa hatua stahiki.
Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa wa chama hicho, Shaweji Mketo, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, maandamano hayo hata kama ikitokea jeshi la polisi ikayazuia, yatafanyika kama yalivyopangwa.
Akielezea kuhusu maandamano hayo, Mketo alisema kuwa, tayari wameshamwandikia barua Rais na jeshi la polisi kuhusu azma hiyo na kwamba Ikulu wanatarajia kupokelewa na Kikwete au mwakilishi wake. Alisema Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova, amempigia simu muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanahabari na kumtaka aende Polisi Kati kwa ajili ya kuandaa njia za kupita siku hiyo.

Alisema maandamano hayo yataanza saa 4:00 asubuhi eneo la Buguruni kituo cha mafuta kuelekea Barabara ya Uhuru, Mnazi Mmoja, Bibi Titi, Posta Mpya, Ardhi na hatimaye Ikulu.
Kuhusu Mtwara, Mketo alisema wanataka kumfikishia Rais malalamiko ya wananchi wa Mtwara kutokana na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na polisi na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Pia alisema maandamano hayo yamelenga kuishinikiza serikali kukomesha vitendo vya kinyama, kijangili vinavyofanywa na majeshi hayo kwa kuwakamata, kuwatesa na kuwabaka wananchi wasio na hatia mkoani humo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment