dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 23, 2013

Pro.Shivji: Mfumo wa dola katika Muungano utakuwa utata

NA MOSHI LUSONZO

23rd June 2013


Profesa Issa Shivji
Kuondolewa kwa jeshi la Polisi katika mfumo wa Muungano na kuzitaka nchi wanachama kuunda vikosi vyao vya usalama, kuna hatari Tanzania ikawa nchi ya kwanza Duniani kuwa na amiri jeshi watatu.
Tahadhari hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji, katika mfululizo wa uchambuzi wa rasimu ya katiba mpya katika mhadhara uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam juzi.
Kwenye kitabu chake cha uchambuzi kinachoitwa `Utatanishi na ukimya katika rasimu ya katiba mpya', Profesa Shivji, alisema kitendo cha kuwaachia nchi wanachama kuunda vikosi vya polisi ni hatari.
Alisema Tume ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya, inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, ni kama imefanya maelewano ili kuhalalisha Idara maalum ya Zanzibar inayojumuisha Jeshi la kujenga Uchumi (JKU), Kikosi maalum cha kuzuia magendo (KMKM) na Chuo cha Mafunzo kuwa kikosi cha ulinzi na usalama.
Profesa Shivji, alisema nguvu hiyo inatokana na ibara ya 227(1) ya rasimu hiyo inayosema "Washirika wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi vitakavyosimamia masuala ya usalama na watu na mali katika maeneo yao."
"Kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa mkuu wa nchi, Kiongozi mkuu wa Serikali ya Mapinduzi, Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, na Kamanda Mkuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama," alisema Shivji.
Alisema Tanzania bara pia itafuata nyayo hizo kwa kuunda vikosi vyao vya ulinzi na usalama na Rais wake atakuwa ndiye Kamanda Mkuu wa vikosi hivyo.
"Kwa hali jinsi ilivyo, vikosi vya Tanzania bara au Tanganyika vitakuwa na uongozi wa kitaalamu, silaha za kisasa na nguvu zaidi kuliko Jeshi la Muungano, ambalo litajikuwa halina fedha za kujiendesha, unadhani nini kitatokea?" alihoji Profesa.
Hata hivo, alisema uwapo wa mahakama ya juu, linatia mashaka kwa sababu rasimu hiyo haionyeshi chombo hicho na mahakama ya rufaa kuwa ya Muungano.
Alisema kimsingi inaonyesha nchi wanachama hazishurutishwi kupeleka kesi zao kwenye chombo hicho na badala yake imependekezwa zinaweza kufanya hivyo endapo zikipenda.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment