NA MWANDISHI WETU
21st June 2013
Uamuzi huo aliutangaza mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya upanuzi wa Chuo cha Mtakatifu Augustine Tawi la Mbeya.
Ni baada ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Peter Chacha kumweleza kuwa kushuka kwa kiwango cha elimu kwa shule hizo nchini kunatokana na baadhi ya shule kuwa na migogoro ya kiutawala.
Jaji Chaha alisema kuwa kumekuwa na migogoro katika shule hizo inayosababisha wanafunzi wengi kufeli katika mitihani yao ya kawaida na ya taifa.
Alisema serikali inatakiwa kufanya uchunguzi katika shule nchini ili kubaini zenye migogoro katika utawala wake.
Alisema kumekuwa na shule ambazo utawala wake umekuwa ukigombania madaraka na kuacha kumpa haki mtoto ya kumfundisha.
“Shule nyingi za binafsi zimekuwa zikijihusisha na migogoro ya kung’ang’a nia madaraka wengine wakitaka ukuu wa shule na wengine ukurukenzi na hata wengine uhasibu, ” alisema Jaji Chacha.
Alimtaka Mulugo kuzitembelea shule binafsi za serikali mkoani Mbeya ili kubaini zenye
migogoro na matatizo mengine ya kitaaluma na kuzifungia ili kuepusha madhara kwa wanafunzi.
Mulugo alisema kuwa atafanya ziara hiyo ya kushtukiza katika shule hizo bila kutaja ni lini ili kubaini matatizo yaliyopo.
Katika harambee hiyo zaidi ya Sh. milioni 100 zikiwamo fedha taslimu na ahadi zilichangwa.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment