dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 23, 2013

Mzindakaya akosoa uundwaji serikali tatu

23rd June 2013


Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwera mkoani Sumbawanga, Chrisant Mzindakaya, ameipongeza Tume ya Katiba mpya, ila amekosoa uundwaji wa serikali tatu iliyopo katika rasimu kwa sababu nchi inaweza kuingia katika mpasuko.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mzindakaya alisema rasimu hiyo haikuwashirikisha Watanzania badala yake ililenga mapendekezo ya viongozi wa tume ya katiba.
“Kama tume itapitisha serikali tatu wakati nchi ina serikali mbili na imeshindwa kuboresha maisha ya wananchi,ibaini kuwa mchakato wa uchaguzi wa urais 2015 hautoweza kutumika kwa sababu bado kutahitajika serikali moja” alisema.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo, aliainisha kuwa ni rahisi kwa seriakli kuboresha tume ya katiba mpya kwa maslahi ya Watanzania kuliko kujibebesha jukumu ambalo linaweza kuingiza nchi katika vita vya mara kwa mara.
“Mapendekezo yangu viongozi wote walioshiriki kuandaa katiba waondoe ubinafsi wa makundi ya kisiasa ili kuwasaidia wananchi kwa sababu hakuna serikali mbili yenye marais watatu duniani kote alisema.
Sambamba na hilo, amewaasa viongozi wote walioshirikiana na hayati Mwalimu Julias Nyerere kukaa pamoja kujadili tatizo la uundwaji wa rasimu kabla hawajavunja muungano uliopo kwa sababu nchi itafia mikononi mwao.
Alisema tume ya viongozi walioshirikiana na Nyerere, ni Mwenyekiti wa tume ya katiba Joseph Warioba, Jaji Mstaafu Mark Bomani, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad , Makamu wa rais Dk Mohamed Gharib Bila, akiwamo Rais Jakaya Kikwete na wengine watano.
“Enzi za uhai wa Nyerere viongozi hao walikuwa mstari wa mbele katika kuunda muungano wa serikali ya Zanzibar na Tanzania, hivyo wawe makini katika hilo kwa sababu mzimu wa Nyerere bado uko hai.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment