dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 15, 2013

RASIMU DAY!!

TANGAZO

Written by   //  14/06/2013

rasimu day
(SAFARI YA MAMLAKA KAMILI INAENDELEA)
Haya haya wazanzibari! Kumekucha! La mgambo likilia kuna jambo! Chama cha wananchi CUF kinawatangazia wanachama, wapenzi na wazanzibari wote wa mikoa miwili ya Pemba, wazalendo na wapenda nchi yao kwa jumla kuhudhuria kwa wingi katika mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 06/07/2013 huko Masota, wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pema. Mgeni rasmi katika Mkutano huo ni Simba wa nyika, tishio la vibaraka wauza nchi yetu, kipenzi cha wazanzibari, mwenye uzalendo wa hali ya juu na mapenzi makubwa kwa Zanzibar na wazanzibari, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. Mkutano utaanza saa 4:00 barabara za asubuhi mpaka saa 12:00 jioni.
Agenda kuu katika mkutano ni jee safari ya kuelekea mamlaka kamili imefikia wapi? ni jinsi gani wazanzibari wanavyopaswa kujipanga kutoka hatua ya sasa na kusonga mbele na safari baada ya rasimu ya Warioba kutoka? Jee hapo ndio mwisho wa safari yetu?
Maswali yote na hayo yatapatiwa majibu pamoja na mambo kadhaa muhimu. Hatumwi mototo!
Shime wazanzibari wote kuhudhuria kwa wingi bila ya kukosa!
TUNATAKA NCHI YETU SASA TUMECHOKA TAFRANI!
HAKI!
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment