zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 19, 2013

China yaaswa kuwekeza sekta ya viwanda Z`bar

NA MWINYI SADALLAH

19th August 2013


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameomba Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kuangalia uwezekano wa kampuni za nchi hiyo  kufikiria kuwekeza katika sekta ya viwanda visiwani Zanzibar.

Balozi Seif alitoa wito huo alipokuwa akizungumza na Balozi mdogo wa China aliyoko Zanzibar, Chen Oilman, ofisini kwake Vuga mjini hapa jana.

Alisema China ilikuwa nchi ya mwanzo kuunga mkono maendeleo ya Zanzibar  baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa kuwekeza viwanda mbalimbali vilivyosaidia uchumi wa Zanzibar.

Balozi Seif alisema viwanda hivyo mbali ya mapato ya serikali, lakini pia vilichangia kutoa ajira kwa kundi kubwa la wananachi wa Zanzibar hasa vijana.

“Vijana wetu wengi walikuwa na ajira za kuendesha maisha yao kupitia miradi kadhaa ya viwanda vilivyoanzishwa na marafiki zetu wa China kama vile Kiwanda cha Sukari Mahonda, Ngozi na Viatu Mtoni na kile cha Sigara Maruhubi, lakini vyote hivyo sasa vimekufa na kuongeza wimbi kubwa la watu wasio na ajira," alisema Balozi Seif.

Alipongeza mchango wa China katika kuharakisha maendeleo ya Zanzibar kutokana na misaada yake katika sekta ya elimu, afya na kuahidi kuwa Zanzibar itaendelea kuimarisha ushirikiano wake.

Naye Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar, Chen Qiiman, alimhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba nchi yake itaendelea kutoa fursa za masomo katika fani mbalimbali sambamba na kusaidia miradi ya maendeleo Zanzibar.

Alisema Wazanzibar wapatao 700 tayari wameshapata mafunzo ya muda mfupi, mrefu na semina mbalimbali ndani ya kipindi cha miaka miwili nchini China, kitendo ambacho kitazidisha kasi ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Kuhusu  ziara ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein nchini China hivi karibuni, alisema imechangia kuamsha ari ya kampuni za nchi yake kuwekeza vitega uchumi vyao Zanzibar.

Balozi Chen alisisitiza kwamba ujumbe wa viongozi na wataalam 20 kutoka  China unatarajiwa kuwasili Zanzibar mwishoni mwa mwezi huu kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika sekta ya uvuvi na utalii.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment