zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 20, 2013

Tutapambana na wanaoturejesha nyuma- Mansoor

Mansoor Yussuf Himid amevuliwa gamba lakini bado hajutii chama chake kumvua gamba anasema 'tunahitaji kuwa na mapinduzi ya fikra'
Mansoor Yussuf Himid amevuliwa gamba lakini bado hajutii chama chake kumvua gamba anasema ‘tunahitaji kuwa na mapinduzi ya fikra’
Mansoor Yussuf Himid Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki (CCM) amesema Zanzibar inahitaji mapinduzi ya kifikra ili wananchi waweze kusonga mbele katika kuiletea mabadiliko nchi yao.
Mansoor amesema hayo leo katika mahojiano yake na Radio ya Dw katika matangazo yaliorushwa saa 7 mchana ambapo alisema ana matumaini makubwa ya wazanzibari kusonga mbele katika kuiletea maendeleo nchi yao katika mchakato wa kupatikana katika mpya nchini Tanzania ambapo alisema anafurahishwa na mijadala inavyokwenda hasa inayohusisha masuala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mwakilishi huyo ambaye hivi karibuni amejinyakulia umaarufu mkubwa kutokana na misimamo yake ya kuitetea Zanzibar amesema wapo watu ambao wana fikra za kudumaza mapambano yanayoendelea ya kutaka mabadiliko katika muungano lakini alisema hawatafanikiwa kwa kuwa wazanzibari watapambana nao.
“Ni kweli wapo watu wenye fikra za kizamani wasiotaka maridhiano wasiotaka mabadiliko na wasioitakia mema Zanzibar lakini tutapambana nao wenye fikra hizo za kihafidhina wenye fikra za kukataa mabadiliko na kukataa maendeleo” alisema Mansoor.
Aidha alionesha kufurahishwa kwake na wimbi la vijana ambao kwa dhati wanaonekana kupata kuleta mabadiliko katika nchi yao huku akisifia hali ya amani iliyopo sasa baada ya kufikiwa maridhiano ya kisiasa kati ya vyama viwili vikuu vya CCM na CUF.
“ Hakuna anayebisha kama hali ya amani iliyipo tunapaswa kujivunia nayo kwa sababu huko nyuma tulikuwa hatuna amani na ilikuwa mtu hajui wakati gani atapigwa au atakutwa na nini watu wakiishi kwa wasiwasi sasa hivi tunapaswa kushukuru kwa hali tulionayo” aliongeza Mansoor.
Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment