Katibu Mkuu wa CUF ambae pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim. Seif Sharif Hamadi akiwatubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalimu Seif Sharif Hamadi amelaani vikali vitendo vya hujuma vinavyofanywa na watu wasiojulikana kwa kuwamwagia tindikali watu wasio na hatia akiwemo Padri hapa Zanzibar.
Alisema kuwa vitendo hivi havivumiliki na kulitaka jeshi la Polisi lifanye kazi zake kitaalamu na kuweza kuwakamata wahusika ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa CUF wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kibanda maiti hiyo juzi.
Aidha alilitaka Jeshi la Polisi wanapotoa maelezo yao kwa vyombo vya habari waweze kutumia lugha nzuri katika kuwapa watu habari juu ya matokeo mbalimbali yanayotokea hapa nchini.
Sambamba na hayo Katibu Mkuu huyo amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kutotia saini mswada wa marekebisho ya rasimu ya Katiba kwani kuna baadhi ya mambo yameingizwa bila ya kushirikishwa upande mmoja wa Muungano
“Rais Kikwete alikuwa na nia nzuri tu kwa kuitangaza azma yake ya kutugnwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika mwaka 2014 lakini kuna baadhi ya watu wachache wasiyoitakia mema Zanzibar”,alisema Maalim Seif.
Alifahamisha kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda alimuandikia barua rasmi Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi ili kiushirikiana kufanya marekebisho ya sheria vifungu sita vya rasimu ya katiba kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili kutoa maoni yake.
Alifahamisha kuwa vifungu vitatu vilionekana kuwa havitoi haki kwa Wazanzibari vikabadilishwa kwa kuwekwa sawa baada ya marekebisho hayo yakafanyika marekebisho mengine manane bila ya kushirikishwa upande wa pili wa Muungano jambo ambalo chama cha CUF hawakuliridhia.
Maalimu seif aliwapongeza wale wote walioshiriki kikamilifu katika mabaraza mbali mbali ya wilaya kwa kuweza kujadili rasimu na kupeleka maoni yao ya marekebisho ya katiba.
Katibu Mkuu wa CUF ambae pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim. Seif Sharif Hamadi akiwatubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar
Chanzo: Maelezo Zanzibar
No comments :
Post a Comment