zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 20, 2013

CUF yataka wahamiaji haramu Zanzibar

NA MWANDISHI WETU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe
 
Chama cha Wananchi (CUF) kimeishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuendesha zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu visiwani Zanzibar kutokana na kuwapo kwa wimbi la wahamiaji hao ili kuweza kupunguza vitendo vya uhalifu ikiwemo matumizi ya mabaya ya tindikali.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa Mawasiliano, Habari na Haki za Binadamu wa chama hicho, Salum Bimani, jana.
Alisema Tanzania ni nchi mbili zilizoungana hivyo zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu linapaswa kuendeshwa nchi nzima na si kwa Tanzania Bara pekee kwani wahamiaji haramu wameenea katika pande zote hususan katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Alisema chama hicho kimeunga mkono zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu linaloendelea Tanzania Bara hivyo zoezi hilo kuihusisha na Zanzibar kwani litasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu ikiwemo matumizi mabaya ya tindi kali ambayo yameshamiri visiwani Zanzibar.

“Inashangaza kuona zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu linafanywa Tanzania Bara peke wakati sisi ni nchi mbili zilizoungana kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Bimani.
Chama hicho kimetoa agizo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kulifanyia kazi suala hilo ili zoezi hilo lisaidie haki kutendeka kwani tayari kuna fununu kwamba baadhi ya wahamiaji haramu waliopo Zanzibar wameshapatiwa vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi na upo uwezekano wa kupiga kura mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Hamad Masoud, aliitaka Zanzibar pamoja na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kulifanyia uhakiki daftari la Wapigakura kabla ya uchaguzi mkuu kutokana na alichodai kuwa daftari hilo lina kasoro nyingi ikiwamo watu wasiokuwa na sifa ya kuandikishwa wameandikishwa katika daftari hilo.
 
CHANZO: NIPASHE
 
Katibu Mkuu wa CUF Hamad Masoud (kati kati) akizungumza na wandishi wa habari kuelezea mambo mbilimbali yanayoendea nchini, kulia ni mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Omar Ali Shehe na kushoto ni Mkurugenzi wa Haki za Binaadam Salum Bimani, katika ofisi ya CUF Vuga mjini Unguja.
Katibu Mkuu wa CUF Hamad Masoud (kati kati) akizungumza na wandishi wa habari kuelezea mambo mbilimbali yanayoendea nchini, kulia ni mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Omar Ali Shehe na kushoto ni Mkurugenzi wa Haki za Binaadam Salum Bimani, katika ofisi ya CUF Vuga mjini Unguja.

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Omar Ali Shehe wa kwanza kulia akielezea kitu kwa wandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga Kura, katika Ofisi ya CUF Vuga mjini Unguja.
Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Omar Ali Shehe wa kwanza kulia akielezea kitu kwa wandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga Kura, katika Ofisi ya CUF Vuga mjini Unguja.
Baadhi ya wandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

No comments :

Post a Comment