zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 9, 2013

Dk. Bilal azitaka benki kutoa mikopo kwa masharti nafuu

NA MWANDISHI WETU

9th September 2013

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharibu Bilal
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharibu Bilal amezitaka benki nchini kuwasaidia wananchi kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu ili kuwawezesha kuondokana na umasikini.

Akitoa rai hiyo wakati akizindua tawi la benki ya UBL jijini Dar es Salaam juzi, ambapo alisema taasisi za fedha zina wajibu wa kuwasaidia wananchi kwa kuwapatia mikopo bila masharti magumu.

Alisema serikali inatambua uwapo wa sekta za fedha na kwamba zina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

Benki hiyo ambayo ipo jijini Dar es Salaam imefunguliwa kwa mara ya kwanza hapa nchini na kwa Bara la Afrika inapatikana Tanzania pekee.

Dk. Bilali aliitaka UBL kufungua matawi katika maeneo mengine hapa nchini ili kuwafikia wananchi wengi zaidi hususani waliopo vijijini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa UBL, Zamees Ghdrey alisema watahakikisha wanawafikia wananchi wengi ili kuwapatia huduma ya kifedha.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment