zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 29, 2013

Majambazi waliovalia kipolisi wapora benki

NA MOSHI LUSONZO

29th September 2013


  Walikuwa saba na silaha za kivita saa 3 asubuhi
  Wajizolea mapesa kimya kimya bila kujeruhi mtu
Majambazi waliovalia sare za polisi wamevamia benki ya I&M jijini Dar es Salaam na kuiba zaidi ya Sh. milioni 50.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3:00 asubuhi kwenye tawi la benki hiyo lililopo kati ya mtaa wa Indira Gandh na Mosque katikati ya Jiji.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema watu waliohusika na wizi huo walikuwa saba, ambapo kati yao walikuwapo waliovalia sare za kipolisi na walikuwa na silaha nzito za kivita.
Alisema watu hao walifanikiwa kuingia ndani ya benki kama wateja, lakini ghafla watu waliovalia sare za kipolisi waliingia na kumteka mlinzi aliyekuwa mlangoni akilinda.
Kwa maelezo ya watu walioshuhudia tukio hilo, walitaja silaha walizotumia majambazi hayo kuwa ni bunduki aina ya `Shotgun machine' (SMG) moja na bastola moja.

Watu hao hao waliamuru wateja na wafanyakazi waliokuwamo ndani wakati huo kulala chini, huku wakiamuru watunza pesa kutoa pesa zote.
Kamanda Minangi alisema tukio hilo lilikuwa katika mazingira ya ukimya kiasi ambacho hakuna mtu aliyegundua kuna wizi unafanyika.
"Baada ya wateja kulala chini, baadhi ya majambazi walikwenda kwenye vyumba vya kutunzia pesa na kuzichukua," alisema Kamanda Minangi.
Alisema tukio hilo lilidumu kwa muda wa takriban dakika tano na kwamba hakuna madhara yaliyotokea kwa wateja.
Baada ya kufanya wizi huo, watu hao walifanikiwa kuondoka wakitumia gari dogo aina ya Noah namba yake haijafahamika na kwenda sehemu isiyojulikana.
Minangi alisisitiza kuwa polisi wanaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watu waliohusika na tukio hilo ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment