zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, September 26, 2013

Mengi kuwalipia ada watoto wasio na uwezo

NA RICHARD MAKORE

26th September 2013


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti cha ubora mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Barbro Johansson Model, Miriam Panja, aliyefanya vizuri katika mitihani ya shule hiyo kwenye mahafali ya 13 ya shule hiyo eneo la Mbezi Luguruni jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni mwanzilishi wa shule hiyo, Profesa Anna Tibaijuka ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mkuu wa shule hiyo, Halima Kamote na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Salomon Odunga.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, ameahidi kutenga Sh. milioni 200 kila mwaka kuanzia Januari mwakani, ili kusaidia kuwalipia ada wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo katika shule ya sekondari ya wasichana ya  Barbro Johansson iliyopo Luguruni, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kadhalika, Dk. Mengi ameahidi kuwapa zawadi  wanafunzi 78 wanaoatarajia kumaliza kidato cha nne mwaka huu ikiwa watafaulu kwa daraja la kwanza kila mmoja.

Dk. Mengi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 11 na maadhimisho ya miaka 13 ya shule hiyo, aliwaambia wazazi, wanafunzi, walimu na wageni waalikwa kuwa  kila mtu mwenye uwezo wa kifedha ana wajibu wa kusaidia wale wasiokuwa na uwezo hususani katika sekta ya elimu. 

Kuhusu moyo wa kusaidia watu wengine, alisema hata mtu awe na mamilioni ya fedha akifa hawezi kuzikwa nayo na kwamba njia nzuri ya kuzitumia ni kuwasaidia wasiokuwa na uwezo ili waweze kupata elimu ambayo itawasaidia maishani mwao.

Dk. Mengi alisema elimu ni njia pekee ya kumsaidia mtoto na kuwataka wanafunzi wanaotarajia kumaliza kidato cha nne mwishoni mwa mwaka huu kuacha kuwa na ndoto ndogo badala yake wawe na ndoto kubwa.

“Maisha yenu nyinyi wanafunzi yapo mikononi mwenu kwa hiyo lazima mkazanie elimu mnayopewa ili iweze kuwasaidia maishani mwenu,” alisema na kuwataka siku zote kusema maneno ya Kiingereza kuwa “I can, I will and I must” yakimaanisha kuwa nitaweza, nitafanya na lazima nitaweza.

Kwa upande wa zawadi alizowaahidi wanafunzi watakaopata daraja la kwanza, Dk. Mengi aliwataka kutumia fursa vizuri na kuahidi kuupatia uongozi wa shule hiyo Sh. milioni mbili ili zisaidie kuwafungulia akaunti wanafunzi wote ili zawadi hizo zitakapotolewa ziingizwe benki moja kwa moja.

Muasisi wa shule hiyo, Profesa Anna Tibaijuka alisema kitendo kilichofanywa na Dk. Mengi sio cha kawaida na kinafaa kuigwa kwa kuwa ametoa mchango mkubwa ambao utaisaidia jamii moja kwa moja.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment