NA IDDA MUSHI
2nd September 2013
Askari hao walichukua hatua hiyo kutokana na wakazi wa kijiji hicho kugoma kufungua barabara hiyo wakishinikiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, kwenda kusikiliza kero za wafugaji kugeuza mashamba yao malisho ya mifugo.
Abiria hao baada ya kukwama kwenye eneo hilo kuanzia saa 3 asubuhi, kufuatia barabara hiyo kufungwa askari hao walifika kwenye eneo hilo na kuwatawanya kwa mabomu baada ya kukaidi amri ya kuwataka waondoke. Baada ya polisi kuwatawanya kwa mabomu ya machozi, walitoa mawe na magogo na kuruhusu msururu mkubwa wa magari yakiwamo mabasi ya abiria kuendelea na safari.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Eliya Ntandu, aliyemwakilisha mkuu wa mkoa, akiambatana na Kamanda wa Polisi Mkoa, Faustine Shilogile, walifika eneo la tukio na kujaribu kuwatuliza wakazi hao waliokuwa wamebeba mawe na chupa bila ya mafanikio.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu, walikubali kufungua barabara hiyo kwa masharti ya kutaka viongozi hao kwenda kwenye mashamba yao kushuhudia uharibifu unaofanywa na wafugaji.
Hata hivyo, baada ya kwenda kwenye mashamba ya wananchi katika Kijiji cha Msongozi, viongozi hao hawakukuta mazao yaliyoliwa, isipokuwa mashamba yasiyo na mimea yalikuwa na kinyesi cha mifugo.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment