zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 2, 2013

`Tutaendelea kulinda amani popote duniani`

NA RAPHAEL KIBIRITI

2nd September 2013


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
Watanzania wameaswa kuwa nyuma ya mashujaa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), pale wanapomwaga damu yao wakati wakitekeleza majukumu katika operesheni za Umoja wa mataifa (UN), kwa kuwa damu yao inamwagika kwa kazi yenye tija.

Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya kuwaongoza viongozi, maofisa, askari na waombolezaji mbalimbali kuuaga mwili wa P 8881 Meja Khatib Mshindo kwenye viwanja vya jeshi vya Lugalo.

Membe alisema kazi inayofanywa na JWTZ kama moja ya nchi iliyotoa wanajeshi katika Brigedi ya kimapigano (FIB) ya Umoja wa Mataifa (Monusco), katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kuwalinda raia na mji wa Goma dhidi ya kundi la M 23 na makundi mengine yenye silaha, ni ya msingi.

Alisema kwa vyovyote ni lazima kuwe na nchi kama Tanzania na nchi zingine zilizochangia askari ndani ya FIB, zinazoikataa hali hiyo na kuchukua hatua, kama iliyochukuliwa, ili kuwaondolea wananchi wa DRC adha wanayoipata kutoka kwa makundi hayo.

Membe alisema kazi inayoendelea kufanywa na Monusco ni nzuri na inabidi iungwe mkono na Watanzania, kwa kuwa kitu kimoja na kusimama nyuma ya wapiganaji wetu, wakati wakiendelea kutekeleza majukumu yao.

“Tuko huko kwa ajili ya ‘noble course’ (Kazi yenye kutukuka), na ndiyo maana tumepata salamu nyingi za rambirambi toka sehemu mbalimbali za dunia, kufuatia kifo cha shujaa wetu. Tumepata toka kwa Katibu Mkuu wa UN na nchi wanachama wa Baraza la Kudumu la Usalama la UN,” alisema.

MWAMUNYANGE ALONGA
Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF), Meja Jenerali Davies Mwamunyange, alisema Meja Mshindo alifariki dunia Agosti 28, saa tisa jioni, baada ya bomu kuanguka kwenye eneo lao la ulinzi na hivyo kumjeruhi yeye na wenzake watano.

Jenerali Mwamunyange alisema Meja mshindo alifariki akiwa njiani wakati akipelekwa hospitali, kwa matibabu.

“Amefariki wakati akitekeleza jukumu kubwa na la muhimu la kulinda amani na kwa kweli ametoa mchango mkubwa kwa Taifa, Afrika na dunia kwa ujumla,” alisema.

Ratiba ya kuuaga mwili wa marehemu ilianza saa 4 na dakika 35 asubuhi, baada ya mwili wa marehemu kuletwa, ukiwa ndani ya gari 5992 JW 12 lilikuwa limeongozwa na gari nyingine ndogo yenye namba 3357 JW11.

Waziri Membe akifuatana na Jenerali Mwamunyange waliwaongoza waombolezaji kwenda kuuga mwili huo na kisha ulisafirishwa kwenda Zanzibar kwa maziko.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment