zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 23, 2013

Shein ahimiza mapambano dhidi ya Ukimwi, dawa za kulevya

NA MWANDISHI WETU

23rd September 2013


Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein ametaka jitihada za kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi nchini na kupiga  vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine vinavyochangia maambukizi hayo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Jamii na Watoto katika eneo la Welezo Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana,  Dk. Shein alisema imebainika kuwa maambukizi mapya ya Ukimwi kwa vijana yanahusishwa na matumzi ya dawa hizo.

“Katika miaka ya hivi karibuni imebainika kuwa maambukizi mapya ya Ukiwmi  yanawakumba zaidi vijana wanaotumia dawa za kulevya hapa nchini, ”  alisema Dk. Shein.
Kituo hicho kimejengwa na Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi  Zanzibar ZAPHA+ kwa msaada wa Taasisi ya Stephen Lewis Foundation ya Canada ambayo ilichangia Sh. milioni 43.65 ambazo ni sawa na asilimia 40.45

Shein alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali na washirika wengine katika mapambano dhidi ya Ukimwi na dawa hizo ili  kuiokoa jamii hasa vijana ambao ni tegemeo la taifa.

Alisema tangu Ukimwi ulipogunduliwa, SMZ  imekuwa ikifanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha Zanzibar haipati maambukizi mapya na kukomesha  unyanyapaa dhidi ya wanaoishi na virusi hivyo.

Akizungumzia kuendelea kupungua kwa misaada ya wafadhili kwa shughuli za Ukimwi, Shein ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutafuta namna bora ya kusaidiana na taasisi kama ZAPHA+ ili kutekeleza majukumu ya mapambano dhidi ya virusi hivyo.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment