Kwa mara nyengine Jumuiya ya Wandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) inaungana na watetezi wa uhuru wa vyombo vya habari kusikitika na uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kufungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania.
Uamuzi wa serikali umetolewa wakati wana tasnia ya habari tunadai uhuru zaidi wa habari, na wakati bado tunalalamikia kufungiwa gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana.
Uamuzi wa serikali umetolewa wakati wana tasnia ya habari tunadai uhuru zaidi wa habari, na wakati bado tunalalamikia kufungiwa gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana.
WAHAMAZA inaamini kuwa adhabu ya kuyafungia magazeti ni kubwa mno na haikusitahiki, na sababu zilizotolewa na serikali kuyafungia magazeti hayo hazitoshelezi.
Tunaamini kwamba njia bora ya serikali kujenga utawala bora wenye kuheshimu sheria ni kutumia mahkama katika malalamiko dhidi ya habari zinatolewa na vyombo vya habari.
WAHAMAZA inatoa wito kwa wadau wa vyombo vya habari nchini kuendelea na harakati za kuitaka serikali kufuta sheria zote zitazotumia kukandamiza vyombo vya habari ikiwa pamoja na sheria ya kufungia magazeti.
Tunataka serikali ibadili uamuzi wake huo wa kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania mara moja, ili wananchi waendelee kupata fursa ya kupata habari zinazochapishwa na magazeti hayo.
Salma Saidi
Katibu WAHAMAZA
Katibu WAHAMAZA
No comments :
Post a Comment