zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 19, 2013

Mkapa: Aliyesoma hujidhihirisha kwa kufikiri na kutumikia umma

NA MWANDISHI WETU

20th October 2013

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amesema mtu aliyesoma na kuhitimu atadhihirika kwa uwezo wa kufikiri na utayari wa kutumikia wananchi wa Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Mkapa aliyasema hayo mjini hapa katika mahafari ya kwanza ya Chuo kikuu cha Askofu Mihayo Tabora (AMUCTA ), chuo kishiriki cha mtakatifu Agostino yalifanyika kwenye viwanja vya chuo hicho mjini Tabora.
Alisema kuwa anahisi jamii kwa sasa ina ari ya kutafuta majibu ya matatizo na changamoto zinazowakabili na kutokana na njaa kubwa ya maendeleo inapendelea kudakia kupata majibu ya haraka haraka kama vile matangazo ya biashara katika radio na runinga, badala ya kuwa tayari kuonesha utayari wa kutumiza wajibu.
Alisema matokeo yake ni malalamiko yasiyoisha na kusahau kwamba subira yavuta heri, na kuongeza kuwa kiini cha matatizo kinapaswa kichunguzwe kwa makini na changamoto ya elimu inavyoweza kukabiliwa.
Alisema kwa njia hiyo wigo wa fikra utapanuliwa na kuweka misingi imara zaidi ya kutatua matatizo yanayozunguka jamii hasa elimu na miundombinu mbalimbali.
Awali mkuu wa chuo cha AMUCTA, Padre Dk. Javenalis Asantemungu, alisema chuo hicho, kilianza rasmi Novemba 2010 kikiwa na wanafunzi 885, ambapo 51 waliahilisha masomo kutokana na sababu mbalimbali wawili walifariki dunia, 116 wamesoma hadi mwisho lakini hawakutimiza vigezo vya kuhitimu. Wahitimu wa jana walikuwa 718.
Padre Asantemungui aliwataka wakazi wa mkoa wa Tabora ambao hawawezi kujiunga na masomo ya asubuhi na mchana chuo kinaendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili kwa muda wa jioni, utaratibu huo umeanza kuitikiwa na watumishi mbalimbali wa serikali na sekta binafsi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment