
§ AMTOLEA
UVIVUMBOWE,ASISITIZA MABADILIKO
Pamela
Mollel na Goodluck Hongo
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Arusha, Bw. Samson
Mwigamba, amesema kutokana na uadilifu wake na mapenzi mema aliyonayo katika
chama, ameamua kuachia madaraka kwa muda ili kupisha uchunguzi dhidi yake.
Bw.
Mwigamba aliyasema hayo Mjini Arusha jana wakati akizungumza na waandishi wa
habari pamoja na kutoa tuhuma nzito dhidi ya viongozi wakuu wa chama hicho
akiwataka waondoke madarakani.
Alisema
viongozi hao wameonesha udhaifu katika mipango ya chama hicho kutaka kushika dola
na kusisitiza kuwa, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Bw. Freeman Mbowe,
ameshindwa kazi ya kukiongoza chama hicho.
“Chama
kimeshindwa katika mambo mbalimbali zikiwemo operesheni zake kutokana na uwezo
wa Mbowe kufikia mwisho, kitendo cha mimi kutoa maoni ya kutaka Mbowe aondoke
katika wadhifa alionao ili aweze kubaki na nafasi ya Kiongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni kinaonekana ni usaliti,” alisema.
Aliongeza
kuwa, siku za nyuma akiwa katika Jimbo la Karatu, mkoani Arusha, Bw. Mbowe
alimpigia debe Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Wilbrod Slaa akidai atakuwa
mgombea urais wa chama hicho mwaka 2015 lakini hakuonekana msaliti wa kauli
iliyozusha sintofahamu miongoni mwa wanachama.
Akizungumzia
sakata la kuenguliwa kwenye nafasi yake kwa madai ya kutoa siri mbalimbali za
chama, alisema Kikao cha Baraza la Uongozi Kanda
ya Kaskazini hakina mamlaka ya kumuengua kwenye nafasi hiyo isipokuwa Kamati
Kuu ya chama hicho.
“Niliacha kazi yenye
mshahara wa sh. milioni 1.9, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) kutokana na mapenzi mema niliyonayo kwa CHADEMA.
“Nimewahi
kukumbana na misukosuko mingi pamoja na kukaa rumande siku saba kutokana na
msimamo wangu wa kuhamasisha mageuzi ya kweli,” alisema Bw. Mwigamba.
Hata hivyo,
alisema yeye ndiye kiongozi pekee ndani ya chama hicho aliyeandika makala
nyingi kuliko kiongozi yeyote kwa lengo la kuhamasisha mageuzi lakini hadi sasa
anahukumiwa kwa msimamo wa kutaka mabadiliko ya viongozi wanaoonesha kushindwa
kukiongoza chama hicho kimalengo.
Kikao cha
baraza hilo kilihudhuriwa na wabunge wote wa Kanda husika akiwemo Mwenyekiti wa
CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kilichofanyika Mjini Arusha.
Alisema tuhuma
dhidi yake ni kutumiwa na baadhi ya viongozi wa chama akiwemo Naibu Katibu
Mkuu, Zitto Kabwe ili kukisambaratisha chama na kufafanua kuwa, madai hayo ni
fikra potofu za kisiasa.
“Tukiwa ndani
ya kikao, nilirushiwa tofali na Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema,
baada ya hapo, red-briged (walinzi wa chama), walinikamata mbele ya Bw. Mbowe,
Mwenyekiti wa chama Kanda ya Kaskazini, Mchungaji Israel Natse, alisimama na
kusema kikao kinaahirishwa ili waweze kunijadili.
“Mbunge Lema hana
utu, anakosea sana kujiita mcha Mungu kwani amekuwa na tabia ya kuwachafua
baadhi ya viongozi wa chama nikiwemo mimi wakati elimu yake ni ndogo,” alisema.
Alisema
alikijenga chama hicho kwa kutumia rasilimali zake bila kuitendea haki familia
yake na kufafanua kuwa, Bw. Lema si mwanachama halisi katika chama.
Aliongeza kuwa,
yeye ni mwanachama hai na Mtanzania safi anayependa nchi yake na chama chake
hivyo kama viongozi wa chama wataamua kumruhusu amwage mchele kwa mambo
yaliyotokea, wamruhusu na hata shindwa.
CHADEMA wazungumza
Akizungumza na
Majira, Ofisa Habari wa CHADEMA, Bw. Tumaini Makene, alisema tukio lililotokea
Mjini Arusha na kusababisha Bw. Mwigamba kusimamishwa uongozi, halina uhusiano
wowote na Bw. Mbowe.
Alisema baraza
hilo la uongozi lilitoa uamuzi wa dharura kutokana na Bw. Mwigamba kuvunja
kanuni, maadili na taratibu za kikatiba za chama hicho kwani mamlaka hayo
wanayo.
“Viongozi wa CHADEMA
ndiyo walioita polisi ili kumuokoa Mwigamba baada ya kukiri makosa aliyokuwa
akituhumiwa na alitia saini mwenyewe kwa dole gumba... katika kikao
kilichomsimamisha Mbowe hakuwepo.
“Huwezi kulifanya
jiwe liwe kichuguu hivyo kinachoelezwa juu ya jambo hili ni propaganda tu dhidi
ya Mwenyekiti wa chama kwani sisi tunaushahidi wa picha za mnato na video,”
alisema.
Aliongeza kuwa, katika kikao hicho hakukuwa na vurugu
ila baada ya Bw. Mwigamba kuambiwa atoke nje na kushindwa kufanya hivyo, ndipo
walipoitwa polisi kwa ajili ya usalama wake mwenyewe.
No comments :
Post a Comment