Spika wa hivi sasa wa Baraza la Wawakilishi ambae
atakuwa wa mwanzo kuikaa hii nyumba mpya!
Written by Harith // 20/10/2013 for Mzalendo Blog
ZANZIBAR.
NYUMBA MPYA YA KISASA YA KUISHI SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI IMEKAMILIKA NA ANATARAJIWA KUHAMIA HIVI KARIBUNI MARA BAADA YA KUKAMILIKA KWA MATENGENEZO MUHIMU YA MIUNDOMBINU YA MAJI SAFI.
HAYO YAMEELEZWA NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS, NDUGU MOHAMED ABOUD MOHD WAKATI AKIJIBU MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI KATIKA KIKAO KINACHOENDELEA HUKO MBWENI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
AIDHA WAZIRI ABOUD AMEBAINISHA KUWA NYUMBA HIYO YAKISASA ILIYOPO MIGOMBANI IMEGHARIMU JUMLA YA SHILINGI BILIONI 1.2 AMBAPO ASILIMIA 62 YA FEDHA HIZO ZIMETOLEWA NA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO NA ASILIMIA 18 NI MCHANGO WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.
AIDHA WAZIRI HUYO AMESEMA KUWA NYUMBA HIYO IMEKAMILIKA KWA ASILIMIA KUBWA AMBAPO KASORO ZILIZOPO NI TATIZO LA UKOSEFU WA MAJI AMBAPO MIUNDOMBINU HIYO KWA SASA INAFANYIWA MAREKEBISHO.
AMESEMA KUWA NYUMBA HIYO IMEJENGWA KWA KUZINGATIA VIGEZO VYOTE VYA NYUMBA ZINAZOSTAHIKI KUISHI WAKUU WA NCHI.
HATA HIVYO MWAKILISHI WA JIMBO LA WAWI NDUGU SALEH NASSOR JUMA ALISEMA KUWA ENEO ILIPOJENGWA NYUMBA HIYO SIO ZURI KUTOKANA NAKUWEPO BARABARANI AMBAPO UTULIVU UNAKOSEKANA.
AKIJIBU SWALI LA NYONGEZA LA MWAKILISHI HUYO WAZIRI ABOUD AMEFAFANU KUWEPO NYUMBA HIYO BARABARANI SI TATIZO KUTOKANA NA NYUMBA ANAYOISHI RAIS WA ZANZIBAR DK ALI 8
Chanzo: Mzalendo
Comments on "SHILINGI BILIONI 1.2 ZATUMIKA KATIKA UJENZI WA NYUMBA YA SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI"
20/10/2013 at 6:06 mu ·
Kwa hapa Unguja 1.2 billion si pesa za kusema pesa hasa kwenye ujenzi. Na isitoshe ati 62% zimetoka kwenye Muungano! Na serikali yetu 18% na 20% zinatoka hewani!
Ni kweli lakini hiyo anayokaa ina tatizo gani? Kuwa serikali igharimike kujenga nyumba mpya ya spika wakati kuna mambo muhimu zaidi.
Panataka kujengwa mnara wa mabilioni wakati maskuli yanaanguka maspitali imekua vituo vya marazi sio vya afya tena,maji hayapatikani wakati wanasema kisiwa kinamaji ndio maana hawajengi nyumba za kwenda juu,hivi kweli serikali ya ccm zanzibar haina muelekeo wala dira.mazumbukuku watupu.
Haya kweli majanga mm nauliza hivi Spika kashakaa muda gani madarakani sasa? Na jee miaka yote alikua anakaa Wapi?Na mshahara na marupurupu aliyokusana hivi hana Nyumba ya kuishi miaka yote hiyo?Na jee hii nyumba iliyojengwa kwa gharama za Serkali ni mali yake?Au ni ya Serkali kwa ajili ya Viongozi? Akistaafu yeye itatumika kwa Kiongozi mwengine au huyo mwengine na yeye atajengewa yake? Kwa kweli inasikitisha saana hii Serkali tulonayo kwa upande wangu mimi naona huu ni msiba mkubwa na Serkali hii yetu HAYA NI MAJANGA.