Dkt. Sengondo Mvungi, aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuzi
Wakati ikiwa ni jana tu ambapo Waziri wa mambo ya ndani Dkt . Emmanuel Nchimbi alitangaza kushikiliwa kwa watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi aliofanyiwa Dkt. Sengondo Mvungi aliyekua mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuzi.
Habari zilizopatikana jioni hii zinasema kwamba mjumbe huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dakta Sengodo Mvungi amefariki dunia majira ya saa tisa alasiri; katika hospitali ya Mill Park huko Afrika ya Kusini alipokuwa akipata matibabu ya majeraha ya mapanga.
Dkt. Mvungi alijeruhiwa kwa kukatwa katwa mapanga kichwani usiku wa kuamkia Jumapili Oktoba 3 Mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mill Park, Johannesburg, Afrika Kusini.
No comments :
Post a Comment