Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 27, 2013

CCM, CUF watifuana

MARIDHIANO yaliyofikiwa baina ya vyama viwili vya CCM na CUF yameingia dosari, baada ya kila upande kutishia kulipiza kisasi dhidi ya kile kilichodaiwa kujeruhiwa kwa wanachama wake.
Wakati CUF wakituhumiwa kutoa kauli za vitisho ambazo zinadaiwa kuchangia kutekwa na kuumizwa kwa watu, CCM imedaiwa kuwa sasa itachukua hatua za kujibu mapigo ikiwa polisi itashindwa kuwakamata watu waliobainika kushiriki katika matukio ya kuvunja sheria.
Jana, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, alisema kuwa wameanza kuishiwa uvumilivu, hasa baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa mwanachama wao Hassan Abdallah Said (25).
Shaka alitoa kauli hiyo jana katika hospitali ya Mnazi Mmoja, alipokwenda kumjulia hali mwanachama huyo.
Mwanachama huyo mkazi wa Jimbo la Mpendae, Mkoa wa Mjini Magharibi, alishambuliwa usiku wa kuamkia Novemba 24 alipokuwa akitoka harusini.
Alisema kwa muda sasa vijana wa CUF wamekuwa wakitoa matamshi yanayoashiria uvunjifu wa amani bila kuchukuliwa hatua, na sasa kumekuwa na ongezeko la matukio ya kupigwa na kujeruhiwa kwa watu, hususan wanachama wa CCM.
“Walitoa matamshi hatarishi, UVCCM tulimjulisha Kamishna wa Polisi Zanzibar tukitaka hatua za kisheria zichukuliwe, tukio hili ni kama yale yale ya kumwagiwa tindikali,” alisema.
Shaka aliyeambatana na msafara wa viongozi waandamizi wa CCM Zanzibar, alisema ikiwa polisi watashindwa kuchukua hatua za haraka, UVCCM hawatosita kukabiliana na matukio hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja alikolazwa, Hassan alisema alikuwa akitokea kwenye harusi majira ya saa sita usiku, mara akavamiwa na vijana watatu waliomuita jina lake na baadae kuanza kumshambulia kwa mapanga.
Alibainisha kuwa aliamua kukimbia ili kujinusuru dhidi ya mashambulizi ya watu hao ambao wawili kati yao aliwatambua kutokana na kuwaona wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kisiasa na kidini.
Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa CUF aliyehojiwa na Tanzania Daima Jumatano, na kuomba asitajwe jina lake gazetini, alisema kuwa tuhuma hizo za CCM dhidi yao ni za uzushi na zinazolenga kuficha ukweli wa kile kinachojiri kuhusiana na usalama wa raia na mali zao kote nchini.
“CCM waache unafiki. Wao ndio wenye dola, lakini sote tunajua namna ambavyo nchi imeingia katika matukio ya kuangamiza watu.
“Wao ndio waulizwe nani anahusika na kuua watu huku Zanzibar na bara, nani anahusika kumwagia watu tindikali, na hadi sasa wameshindwa kukamata watu wanaohusika badala yake wanabambikia watu kesi,” alisema kiongozi huyo.
Alidai kuwa CUF haina sababu ya kujiingiza katika matukio kama hayo, kwa sababu hawana dola na hawaamini katika kuendesha siasa za majitaka, kuua na kujeruhi watu.
Kuumizwa kwa kada huyo wa CCM ni moja tu ya matukio mengi yaliyokwishatokea visiwani hapa.
Mapema mwaka huu, Padre wa Kanisa Katoliki, alipigiwa risasi na kuuawa, wakati mwingine akijeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa tindikali.
Kadhalika, kiongozi mwingine wa Kiislamu alimwagiwa tindikali, na mwingine akikutwa amenyongwa katika shamba lake.
Hata hivyo, hadi sasa Jeshi la Polisi limewakamata watu wachache na kuwafikisha mahakamani wakituhumiwa kuhusika na matukio hayo.
Chanzo: Tanzania Daima

No comments :

Post a Comment