zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, November 1, 2013

Huawei kuzisaidia shule 150 nchini

NA MWANDISHI WETU

22nd October 2013

Kampuni ya Huawei ya China
Kampuni ya Huawei ya China ina mpango wa kuzisaidia shule za sekondari 150 nchini kupata mafunzo kwa njia ya mtandao wa mawasiliano (E-Education) kama njia ya kukabiliana na uhaba wa walimu na vitabu vya masomo.

Hayo yalisemwa juzi na Rais wa kampuni hiyo, William Xu wakati wa  mazungumzo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye makao makuu yake jijini Shenzhen, China.

Alisema walipokea maombi ya serikali ya Tanzania ya kusaidia Mkongo wa Mawasiliano ya Taifa (NCITBB) ili kuinua kiwango cha elimu ya watoto wa Kitanzania. Kampuni ya Huawei ndiyo iliyojenga mkongo huo.
Alisema kwa kuanzia, mradi huo utazihusu shule 50 ambapo shule mbili kutoka kila mkoa zitaunganishwa kwenye mtandao zikiwa na madarasa ya kujifunzia teknolojia mpya (multimedia classrooms), maabara ya kompyuta (computer lab),  projekta, mafunzo ya kwenye mtandao yanayofundishwa kwa njia ya video, (Online video teaching) na (online applications).

“Shule nyingine 100 zimekwishaainishwa lakini zenyewe hazitakuwa mtandaoni moja kwa moja, bali katika awamu ya pili zinaweza kuunganishwa na kuwa mtandaoni kutegemea na upatikanaji wa intaneti na kasi yake.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment