NA SALOME KITOMARY
31st December 2013
Akizungumza jana wakati wa makabidhiano ya rasimu ya pili ya katiba, aliwataka wananchi kutoa maoni yao kupitia wawakilishi wao watakaounda Bunge Maalum la Katiba.
Aidha, aliwapongeza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kukusanya maoni, kuchambua maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya kwanza na pili na sasa ipo katika hatua ya mwisho.
Alisema wananchi walifarijika sana walivyopokea rasimu ya kwanza ingawa vipengele vingine hawakuona kama vipo kwa matakwa na mahitaji ya yo, lakini Tume hiyo imefanya kazi yake.
Aidha, alivipongeza vyombo vya habari kwa kazi kubwa ya kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kutoa maoni yao ili kufanikisha upatikanaji wa Katiba mpya.
Dk. Shein alimpongeza aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadilikoya katiba, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi, akisema kuwa alitoa mchango mkubwa na kuwataka Watanzania kumkumbuka na kuenzi mchango wake.
Dk. Shein pia alisema kuwa serikali kupitia mchakato wa katiba imejifunza kuhusu kero mbalimbali zilizoko katika Muungano.
Aliwataka wananchi wote kushiriki katika mchakato wa kupata katiba mpya kwa amani na utulivu.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment