NA THOBIAS MWANAKATWE
23rd December 2013
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willibrod Slaa, alisema hayo jana wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi mji wa Bukene na kijiji cha Lusu wilayani Nzega.
Dk. Slaa alisema baada ya mawaziri wanne kuwajibishwa kinachotakiwa iwe ni zamu ya Waziri Mkuu, Pinda kuachia ngazi na kwamba iwapo hatajiuzulu wabunge wampigie kura ya kutokuwa na imani naye.
“Matatizo yaliyojitokeza wakati wa Operesheni ya Tokomeza Ujangili Waziri Mkuu kama bosi wa mawaziri anapaswa kuwajibika na siyo kuacha mawaziri wanne tu ndio wawajibishwe,” alisema.
Alisema Waziri Mkuu anatakiwa kuachia ngazi kwa sababu mambo mabaya na unyama waliofanyiwa wananchi na mifugo wakati operesheni hiyo ni matokeo ya kauli yake aliyowahi kuitoa Bungeni kwamba sasa serikali imechoka ni kupiga tu.
Dk. Slaa alisema idadi kubwa mawaziri katika serikali ya awamu ya nne ni mzigo isipokuwa wawili tu ambao hata hivyo, hakutaja majina yao.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment