NA ASHTON BALAIGWA
15th December 2013
“Sisi mawaziri tunatukanwa sana pale bungeni kama watoto kwa ajili yenu nyie watendaji mnaoshindwa kutimiza majukumu yenu lakini tunashindwa kuwataja tu, sasa kuanzia sasa anayeona hawezi kufanya kazi aondoke mapema vinginevyo mimi siwezi kukubali kutukanwa kwa ajili yake," alisema Nahodha.
Alisema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kinachofanyika mjini hapa kwa siku mbili ambalo linahudhuriwa na wajumbe ambao ni wawakilishi wa taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo.
Alisema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kinachofanyika mjini hapa kwa siku mbili ambalo linahudhuriwa na wajumbe ambao ni wawakilishi wa taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo.
Alisema kuwa wakati anapewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo aliulizwa kama ataweza na alijibu anaiweza na kueleza vitendo vya kuendelea kusemwa bungeni kutokana na uzembe wa baadhi ya watumishi hawezi tena kuvumilia na badala yake kabla ya yeye kusemwa atahakikisha huyo aliyefanya uzembe anachukuliwa hatua ikiwemo na kuondolewa kazini.
“Kama kuna mtu anaona ana kazi nyingi hawezi kutekeleza majukumu ya wizara aniambie kabisa hapa ili atolewe, lakini siyo mnisababishie mimi kutukanwa kule bungeni kwa uzembe wa mtumishi wa wizara hii nasema wazi sitokubali katika hili,” alisema Nahodha.
Aliwataka watendaji wa wizara hiyo kumpa na kutoa maelezo ya wafanyakazi 200 waliotakiwa kupandishwa vyeo mwaka jana na kama wapo wasiopandishwa apewe ni sababu zipi zimewafanya wasipewe vyeo.
“Mwaka jana mliniambia mnapandisha vyeo wafanyakazi 200 baadaye mkaahirisha mkasema mwaka huu sasa nataka idadi ya waliopandishwa wangapi na wasiopandishwa na sababu zake nizipate, hatuwezi kuzungumzia maslahi ya wafanyakazi huku wengine wakiendelea kuneemeka na wengine wakiumia,” alisema.
Akizungumzia miradi mbalimbali ya wizara hiyo, waziri Nahodha alisema kiwango cha usimamizi wa miradi hiyo ipo chini na kutaka watendaji hao kutoanzisha miradi mipya katika mwaka ujao wa fedha mpaka wakamilishe iliyopo sasa.
Akizungumzia baraza hilo la wafanyakazi, alisema lina umuhimu mkubwa kwa kuwa ndiyo chombo pekee cha kurekibishana na kudai maslahi ya wafanyakazi pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya wizara.
Awali Katibu mkuu wa Wizara hiyo, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo, Job Masima, alisema ni chombo huru cha kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili wizara hiyo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
umtimuwe nanini wewe kamtishie maido vitendo vya uhalifu ni vingi tu na huna chochote ufanyalo .
ReplyDelete