NA JOHN NGUNGE
19th December 2013
Alikuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara kwa kipindi cha Machi hadi Desemba 15, mwaka huu.
“Kumekuwa na matumizi makubwa ya Dola, lakini BoT kama wasimamizi wanaonekana kushindwa kufanya hivyo, na tumeendelea kuona matumizi ya dola sambamba na Shilingi katika manunuzi ya bidhaa nchini.
Matumizi hayo ya dola yanaua uchumi wetu.
Aliongeza: “Hakuna nchi yoyote inayofanya mambo kama tunayofanya sisi hapa, hoteli nazo zinauza bidhaa na huduma kwa dola.” alisema.
Alisema fedha za Dola sasa hivi zinauzwa kama karanga bila udhibiti wowote jambo ambalo nchi zingine hawafanyi hivyo.
Alisema hata katika kikao cha Bunge la Bajeti kilichopita, Waziri wa Fedha, William Mgimwa, alizungumzia tatizo la matumizi ya Dola sambamba na Shilingi.
Alihoji kama Gavana wa BoT ameshindwa kusimamia na kudhibiti tatizo hilo pamoja na Waziri wa Fedha.
Naye Mbunge wa Mkanyageni, Mohammed Habib Mnyaa (CUF), alizungumzia suala la matumizi ya Dola nchini na kutaka lidhibitiwe.
Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM), aliitaka serikali kuweka mkakati maalum wa kufufua viwanda.
“Tunatakiwa kuvifufua viwanda vyetu, serikali itazame jambo hili kwa jicho la pekee,” alisema na kuongeza, “mchango wa viwanda katika Pato la Taifa ni asilimia 25 tu na inatakiwa walau tufikie asilimia 75.”
Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama (CCM), alitaka Serikali kuhakikisha inatekeleza sera yake ya kuvilinda viwanda vya ndani.
Alisema kumekuwa na bidhaa nyingi kama vile sukari ambayo huingizwa nchini kwa wingi na hivyo kuathiri soko la sukari ya ndani.
Hoja ya kutaka sera ya kulinda viwanda itekelezwe iliungwa mkono pia na Mbunge wa Singida Magharibi, Mohammed Missanga (CCM), ambaye alisema zamani enzi za Mwalimu Julius Nyerere, viwanda vya ndani vilikuwa vinalindwa.
Mbunge wa Viti Maalum, Pindi Chana (CCM), alitaka serikali kuwa na takwimu ya viwanda vyake na inatarajia kuwa na vingapi.
Alisema wakati malighafi zipo za kutosha kama vile Mchuchuma na Liganga lakini uanzishaji wa viwanda hufanywa kwa kusuasua.
Alihoji iweje Tanzania ambayo ina sera ya Kilimo Kwanza ishindwe kutengeneza hata majembe ya mkono ambayo kwa sasa yanaagizwa kutoka nje ya nchi.
Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul (Chadema), aliomba Serikali kusitisha matumizi ya kutumia Mashine za Kieletroniki (EFD), katika kutoa risiti za Ankara za kodi badala ya kutumia vitabu kwa sababu zinamnyonya mfanyabiashara.
Alisema gharama za mashine hizo ni kubwa, pamoja na karatasi zake kwa ajili ya kutolea risiti huuzwa ghali na inapoharibika pia gharama ya matengenezo yake ni kubwa pia.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment