Warioba: Apotosha mambo kuhusu
Zanzibar ili kutoa sura nzuri ya Rasimu yapili ya Katibu!
Written by abdisalum
Asalama Alaykum
Kwanza, habari za siku nyingi sana waheshimiwa wa mzalendo. Nilipotea kidogo kwa sababu nilikwenda kuchuma karafuu Bahanasa, na vikataa vyangu vyengine vipo pale Mzabarautakawa.
Jana nimemsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, kuna mambo mengi amesema – na mengine ameyapatia na nimesifu kidogo kwa kusema ukweli; na nimemsifu kidogo kwa kukubali kulitaja neno ‘Tanganyika’ kama mimi nilivyowahi kutoa maoni maana niliuliza ‘tume inaogopa nini ulitaja na kulitia neno Tanganyika’ katika rasimu 1 and 2. Hizo tatu atakuwa nani na nani na nani?? Nimefurahi at least, this time, limeingizwa (ingawa kwa woga, na kinyemela nyemela); maana mara utaona ‘Tanzania Bara’ mara Tanganyika…..hii iwe ajuari: tuseme na tuandike Tanganyika tu — maana ndio nchi tuliyoungana nayo kisheria, sio T.Bara.
Ninachotaka kusema leo ni upotoshaji mdogo alioufanya Warioba, na hili naomba hao wabunge wa katiba watapochaguliwa walisimamie sana kwa ukali wote, na tujue ukweli halisi:
1. Warioba amesema kuwa sasa Zanzibar inaweza kujiunga na FIFA (hili sikweli) kwa sababu FIFA hawachukui nchi kama Zanzibar iliyoungana, wanachama wanakuwa ni ‘sovereign state’. Katika rasimu hii Zanzibar haikutajwa kama ni ‘sovereign state’; unless itaje hivyo kwa mapana na marefu. Jamani, tumeelewena hapo: FIFA haitaki Warioba wala Jamala Malinzi kuingiza Zanzibar uwanachama wake, ni criteria ya ‘nchi/sovereign state’.
- Hapa inabidi rasimu hiyo ibadilishe kifungu hichi na kutamka bayana status ya Zanzibar kama NCHI.
- Kwa rasimu hii FIFA hawakubali
- Hapa inabidi rasimu hiyo ibadilishe kifungu hichi na kutamka bayana status ya Zanzibar kama NCHI.
- Kwa rasimu hii FIFA hawakubali
2. Si FIFA tu, hata Jumuiya ya Afrika Mashariki para 1 inasema wao wanaojiunga ni ‘nchi kamili/sovereign state’ so Zanzibar kwa charter ya EAC haiwezi hata kujiunga kama affiliated member, seuze FIFA. Msifike mbaaaaali sana jama kwenda Geneva, hapo Arusha kwenye makao makuu ya Afrika Mashariki sisi hatuthubutu kutia mguu wetu. Huu ndio ukweli.
- Hivi hili hawakuliona? Tuseme hawalijui, tuseme wajumbe wetu kutoka Zanzibar hawajui hili (hee basi…hatari)
- Hivi hili hawakuliona? Tuseme hawalijui, tuseme wajumbe wetu kutoka Zanzibar hawajui hili (hee basi…hatari)
Nini tufanye: Hatujachelewa……….wajumbe wa bunge la katiba la zanzibar kama watakuwa smart enough, wanaweza kurekebisha hili. Na hili nimewasaidia, na naomba walichukue kama wako tayari — au kama ndio wanasubiri posho nono, nchi inazidi kuteketea.
OMBI langu kwenu: tuitafute charter ya EAC tuisome, inasemaje
Tuitafute statue ya FIFA inasemaje?
Wajumbe wa Zanzibar wafanye reference kama hizi na nyenginezo jamani
Tuitafute statue ya FIFA inasemaje?
Wajumbe wa Zanzibar wafanye reference kama hizi na nyenginezo jamani
Kadhalika, OIC nafikiri na wao wamebadilisha katiba yao, sifikiri kama Zanzibar inaweza kuwa mwanachama wa moja kwa moja — ila hili sina hakika nalo sana 100%, nitalitafuta zaidi au analelijua pia atuarifu — tusivamie tu.
Mimi nafikiri kuwa hapa tulipofika, tuwasaidie hao wataochaguliwa, tuwape mawazo na tuwape vidokezo/documents ili ziwasaidie. kama wako tayari kusaidiwa: hii rasimu 2 — bado sana, mimi naona hata 30% haijafikia demands zetu, imejaa ujanja ujanja mwingi — take one example: mambo ya Uraia na ulinzi….haya tu yanaweza kutukumoa.Yanaweza kuidhibiti Zanzibar hata kama tutapewa kila kitu. Be careful…..!
Chanzo: Mzalendo.net
No comments :
Post a Comment