Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, May 16, 2014

BENJAMIN MKAPA NA MKEWE WATUA MAREKANI!

BALOZI LIBERATA MULAMULA AMKARIBISHA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA MKEWE CHAKULA CHA JIONI NYUMBANI KWAKE

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akimkaribisha Rais mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa mara tu alipowasili nyumbani kwa Balozi Bethesda, Maryland kwa ajili ya chakula cha jioni na kupata fulsa ya kukutana na marafiki zake wa siku nyingi, siku ya Alhamisi May 15, 2014. Mhe. Benjamin Mkapa amekuja Marekani kwa ajili ya mkutano wa African Wildlife Foundation (AWF) uliofanyika Washington, DC.

 Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akitia saini kitabu cha wageni nyumbani kwa Balozi Liberata Mulamula.

 Balozi Liberata Mulamula akimmuonyesha chumba chenye luninga Mhe. Benjamin Mkapa na mkewe wakikumbukia walipokuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo mwaka 1983-1984 wakati alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.


Rais mstaafu Mhe, Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula alipokuwa akiongea machache na kumpa salamu za Watanzania nchini Marekani na jambo kubwa ambalo Balozi Liberata Mulamula alilosisitiza ni kilio cha Diaspora kuhusu swala la uraia pacha. Mhe. Benjamin Mkapa yeye aliongea kwa kumshukuru Balozi Liberata Mulamula kwa kumkaribisha na kutoa salamu toka nyumbani na kuelezea ujio wake Washington, DC.

 Rais mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakifanya mazungumuzo na mwenyeji wao Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

 Juu na chini ni Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na msafara wa Mhe. Benjamin Mkapa wakifuatilia mzungumuzo hayo.



 Juu na chini ni Balozi Liberata Mulamula akiwa na wageni wake, Rais Mstaafu awamu ya tatu Mhe. Banjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa pamoja na marafiki zao wa siku nyingi Toyin Rose na mumewe ambao wanaishi Bethesda, Maryland wakiwa meza ya chakula.



Rais mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akipokea zawadi ya kitabu toka kwa Afisa Mindi Kasiga.


Mama Anna Mkapa akipokea zawadi ya viatu kutoka kwa Afisa Mindi Kasiga.

 Picha ya pamoja ya Balozi Liberata Mulamula na Mhe. Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakiwa pamoja na marafiki zao wa siku nyingi Bi.Toyin Rose(kushoto) na mumewe. 

 Picha ya pamoja Mhe. Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa pamoja na mwenyeji wao Mhe. Libarata Mulamula.

Picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi.

 Balozi Mulamula akiwasindikiza wageni wake Mhe. Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa walipokua wakiondoka.

SOURCE: VIJIMAMBO

No comments :

Post a Comment