Na Daniel Mjema, Mwananchi
Posted Ijumaa,Juni27 2014 saa 9:14 AM
Posted Ijumaa,Juni27 2014 saa 9:14 AM
KWA UFUPI
- Asema kazi zake zimetwaliwa na Baraza la Mapinduzi, amshukia Jaji Warioba
Moshi. Mwanasiasa wa siku nyingi, Peter Kisumo amesema Baraza la Mapinduzi Zanzibar aliloliacha Rais wa Kwanza wa visiwa hivyo, Abeid Aman Karume limeuawa kimyakimya.
Kisumo alisema jana kwamba baada ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar, nafasi ya baraza hilo imechukuliwa na Baraza la Mawaziri Zanzibar.
Akizungumza kwa simu kutoka wodi ya wagonjwa wa moyo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa, Kisumo alisema: “Nataka Shein (Rais Dk Ali Mohamed) aniambie kutoka moyoni mwake kama Baraza la Mapinduzi Zanzibar lingalipo? Kama lipo ni nini mipaka ya Baraza la Mawaziri Zanzibar?”
Waziri huyo katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, ambaye alirejea nchini wiki mbili zilizopita kutoka India alikokwenda kwa matibabu ya moyo na figo alisema mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar 1964, Karume alitembelea Tanzania Bara akiwa na Thabit Kombo na walichagua kutembelea Mkoa wa Kilimanjaro... “Wakati huo nikiwa mkuu wa mkoa nikawapeleka Usseri, Kituo cha Afya wakati huo kilikuwa sawa na hospitali.
Pale nilimsikia ‘Sisi Wazanzibari tumekubali kuungana na Tanganyika... Mapinduzi haya Daima, Mapinduzi milele’, hapo ndipo mwanzo wa kusikia neno Mapinduzi Daima.”
Kisumo alisema anachokiona leo ni mabadiliko kiasi kwamba Baraza la Mawaziri Zanzibar ndilo limeshika hatamu badala ya Baraza la Mapinduzi aliloliacha Karume.
“Swali langu ni kwamba ni azimio gani lilifuta Baraza la Mapinduzi ambalo ndicho kilikuwa chombo cha juu? Karume alisema Mapinduzi Daima bila mapinduzi hakuna Zanzibar,” alisema Kisumo.
Alielezea kushangazwa kwake na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kutouona uasi huo uliofanywa kimyakimya wakati akikusanya maoni ya Wazanzibari.
Mara kadhaa, Jaji Warioba amenukuliwa akisema mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanyika mwaka 2010 yaliyosema Zanzibar ni nchi, yalivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Mabadiliko hayo yalisema Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyozungukwa na bahari yake.
Wakati Katiba ya Zanzibar ikieleza hivyo, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 1 inaeleza kuwa Tanzania ni nchi moja na eneo lake la mipaka ni kuanzia Tanzania Bara hadi Visiwani.
Kifungu cha 2(a) cha Katiba ya Zanzibar kimempa uwezo Rais wa Zanzibar kuigawa Zanzibar katika mikoa na wilaya kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Kisumo amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa siku ya nne jana, akisumbuliwa na maradhi ya moyo pamoja na figo, hata baada ya kurejea kutoka nchini India kwa matibabu.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Kisumo--Baraza-la-Mapinduzi-Z-bar-limeuawa-kimyakimya/-/1597296/2363298/-/142aauhz/-/index.html
.
Huyu Kisumo ana nini jamani? Ndio anasema nini? Hivyo yeye hajui kama Baraza La Mapinduzi ndio Baraza La Mawaziri? Anajitia pressure ya bure huko hospitali. Atuachie mambo yetu Waznz wenyewe.
ReplyDeleteMola ampe shifaa ya haraka na aache kutiatia mdomo mambo ya Unguja!
Wakati wake umepita!!!
Mnafiki mkubwa huyu. Atwambie wapi mkataba wa muungano uliposema Tanzania ni nchi moja. Anashangaa kuuliwa kwa Baraza la Mapinduzi tu kwa nini asishangazwe kuvurugwa kwa makubaliano ya muungano waliokubaliana Nyerere na Karume?
ReplyDelete